Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha ATC Dkt Mussa Chacha akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Umahiri wa Kufua umeme na ufundi umeme Kikuletwa Kijiji cha Chemka Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro
.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa akiongea wakati alipotembelea ujenzi wa kituo Cha Umahiri wa ufundi umeme na bwawa la kuzalisha umeme Kikuletwa kinachoendeshwa na Chuo Cha Ufundi Arusha wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro mapema mwishoni mwa wiki.
.Mkuu wa Wilaya ya Hai akikagua Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Umahiri wa Kufua umeme na ufundi umeme Kikuletwa Kijiji cha Chemka Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kinachoendeshwa na Chuo Cha Ufundi Arusha.
Sehemu ya Watumishi wa Chuo Cha Ufundi Arusha ATC wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Kituo Cha Umahiri wa ufundi umeme na kituo Cha Kufua umeme Kikuletwa Kijiji cha Chemka Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro
……………………………….
Na Ahmed Mahmoud
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha bilion 37 kwa ajili ya
kufufua Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme kilichoanzishwa mwaka 1930
cha Kikuletwa pamoja na chuo cha Ufundi wa umeme na mitambo
kitakachochukuwa zaidi ya wanafunzi 600 ambacho kinaenda kuzalisha
wataalamu watakaotekeleza Miradi ya kimkakati ikiwemo bwawa la Mwalim
Nyerere JNHPP.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Amiri Mkalipa
alipotembelea mradi unaotekelezwa na Chuo cha Ufundi Arusha ATC
ambao utazalisha megawati 1.65 katika kijiji cha Chemka Kikuletwa
wilayani hai mkoani Kilimanjaro ambapo.
Amesema kwamba Mradi huo utakapokamilika utasaidia chuo kuuza umeme na wananchi wanaozunguka kunufaika na huduma hiyo jambo ambalo kituo hicho kitazalisha wataalamu ambao watasaidia katika miradi mbalimbali itakayotekelezwa na serikali hapa nchini.
“Katika utekelezaji wa mradi huu lazima mhakikishe uzalendo unawekwa
mbele sanjari na matumizi sahihi ya fedha bila kusahau kumaliza ujenzi
ndani ya muda uliopangwa ili manufaa ya Kituo hichi yaweze kuwanufaisha kizazi kijacho tofauti na awali ulipotekelezwa”
Awali akitoa Taarifa ya Mradi huo Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha ATC
Dkt.Mussa Chacha alisema kuwa mradi huo wa kituo cha umahiri kuzalisha Wataalamu wa nishati jadidifu watakaokuwa na uwezo wa
kufanyakazi na kuzisaidia nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na
duniani kote kwenye miradi mikubwa ya umeme ya kimkakati.
Amesema kwamba mradi huo unatarajiwa kumalizika mwezi wa oktoba mwaka.2024 huku akimtaka mkandarasi kuendeleza kazi kwa kasi ili kuweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa sanjari na kuhakikisha wanailipa halmashauri mapato yake.
“Tumejipanga kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya muda uliopangwa
sanjari na maagizo ya mh.Mkuu wa wilaya ya hai yanatekelezwa kwa
haraka ili kuondoa changamoto za mapato ya halmashauri ambayo
mkandarasi hajalipa tokea kuanza ujenzi wa chuo”
Kwa Upande wake Mjukuu wa Mmoja ya waanzilishi wa Kituo hicho cha
kuzalisha Umeme Kikuletwa aliyefika kutembelea ambacho kilijengwa
mwaka 1930 na wajerumani WOLF LEACK kutoka ujerumani amesema kwamba Babu yake alikuwa mkandarasi alietekeleza mradi huo wa kituo cha
kuzalisha umeme ambapo baba yake alizaliwa hapa nchini mkoani
Kilimanjaro wilaya ya Moshi mwaka 1936 wakati wa Ujenzi wa kituo.