Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akipokelewa na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei Bw. Zhang, Alipoongoza ujumbe wa Tanzania kutembelea Kampuni hiyo mjini Beijing, China, na kujadili masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania. Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania-China- Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mkuu wa Shirila la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa-Bw. Japhet Justine na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melkizedeck Mbise
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mawasiliano ya Huawei Bw. Zhang, kuhusu shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo, ambapo pia wamejadili masuala ya uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Tanzania. Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania-China- Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mkuu wa Shirila la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa-Bw. Japhet Justine na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melkizedeck Mbise
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Beijing, China)