Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akichimba msingi pamoja na wananchi katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali iliyopewa jina lake ambayo inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP katika kata hiyo Wilayani Chamwino.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na wananchi wa Kata ya Manchali Wilayani Chamwino alipowasili katika kata hiyo kwa ajili ya kushirikiana nao kuchimba msingi katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali iliyopewa jina lake ambayo inayojengwa jimboni kwake kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Kata ya Manchali Wilayani Chamwino alipowasili katika kata hiyo kwa ajili ya kushirikiana nao kuchimba msingi katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali iliyopewa jina lake ambayo inayojengwa jimboni kwake kupitia mradi wa SEQUIP.
Sehemu ya wananchi wa Kata ya Manchali Wilayani Chamwino wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipowasili katika kata hiyo kwa ajili ya kushiriki kuchimba msingi katika Shule za Sekondari zinazojengwa jimboni kwake kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde akiwapongeza wananchi wa Manchali kwa kushirikiana na Mhe. Ndejembi kuchimba msingi wa shule za sekondari zinazojengwa na Serikali katika kata hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akichimba msingi pamoja na wananchi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Dodoma ambayo inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP kwenye kata hiyo Wilayani Chamwino.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kata ya Manchali Wilayani Chamwino alipowasili katika kata hiyo kwa ajili ya kushirikiana nao kuchimba msingi katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali iliyopewa jina lake inayojengwa jimboni kwake kupitia mradi wa SEQUIP.
Na: James Mwanamyoto (OR-TAMISEMI).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi ameshirikiana na wananchi wa kata ya Manchali kuchimba msingi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Manchali itakayoitwa Ndejembi pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Dodoma inayojengwa katika kata hiyo kupitia mradi wa SEQUIP.
Mhe. Ndejembi amesema, wananchi wa Kata ya Manchali wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa shule hizo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha elimu nchini.
Mhe. Ndejembi amefafanua kuwa, ushiriki wa wananchi unapunguza gharama za ujenzi na kuongeza kuwa lengo lake ni kuhakikisha shule ya Sekondari ya Ndejembi inakamilika na fedha inabaki, ikizingatiwa kuwa wananchi wamempa heshima kwa kuipa shule hiyo jina lake kwa kuthamini mchango wake.
Akizungumzia jitihada za kupunguza gharama ya ujenzi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana inayojengwa, Mhe. Ndejembi amesema uongozi wa halmashauri umemtafuta mzabuni wa kufyatua tofali ambaye amefungua kiwanda cha kufyatua tofali kwa gharama nafuu ya shilingi 1400 kwa tofali kwenye eneo ambalo shule hiyo inajengwa.
Aidha, Mhe. Ndejembi amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kujenga wa shule hizo katika kata ya Manchali, shule ambazo zitatatua changamoto ya wanafunzi wa eneo hilo na maeneo jirani kutembea umbali mrefu ili kupata elimu.
“Rais Samia tangia aingie madarakani amefanya mambo makubwa kwa wananchi wa jimbo la chamwino kwani kila eneo ametoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa ajili ya kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Elimu), Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Msonde amewapongeza wananchi wa Manchali kwa kushiriki kuchimba msingi wa shule za sekondari zinazojengwa na kuongeza kuwa, ushiriki wao ni ishara ya kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Mheshimiwa Rais kuboresha elimu nchini.