Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju, ametembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia kilichopo Temeke, Dar es salaam ambapo amepokea Salamu za Mhe. Zainab Goronya Jaji Mfawidhi Kituo Jumuishi Masuala ya Familia na kupongeza namna ambavyo wizara kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii wanavyoshirikiana na Mahakama upande wa huduma za ustawi wa jamii kuhakikisha wateja wanapata haki kwa wakati.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu ameshukuru Kituo Jumuishi kwa kasi ya kusikiliza mashauri na kuahidi wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa kuongeza nguvu kwenye utoaji huduma ya msaada wa kisaikolojia.
Aidha katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu alipata muda wa kutembelea Makao ya Watoto Upanga pamoja na Makao ya Watoto Kurasini. Viongozi wengine waliokuwepo kwenye ziara hiyo ni Naibu Msajili Mhe. Martha Mpaze pamoja na Mtendaji wa Kituo Jumuishi Bw. Samson Mashalla.