Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine pichani ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika Dkt. Olusegun Ogunsanya, Mtendaji Mkuu wa Airtel Tanzania Dinesh Balsingh pamoja na viongozi wengine wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akielekea kuzindua Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika cha Kampuni Mawasiliano na Simu za mkononi ya Artel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakati akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye kuhusu Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini wa 2Afrika kabla ya kuuzindua katika Kituo hicho cha Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo kuhusu Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika kabla ya kukizindua rasmi kwenye hafla iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati wakimuangalia Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza kwenye kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Ubunifu wa Msanii Mrisho Mpoto wakati akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa nembo ya 5G kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika Dkt. Olusegun Ogunsanya mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Roboti akiwa amebeba nembo ya 5G mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania kwenye hafla iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa Mawasiliano kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Artel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
…….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amezindua Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G ambao una urefu wa kilometa 45,000 na uwezo wa kutumiwa na watu zaidi ya bilioni tatu pamoja na kuunganisha Bara la Asia, Ulaya na Afrika
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam leo 10 Agosti, 2023, Rais Mhe. Dkt. Samia, amesema kuwa teknolojia ya 5G itarahisisha utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo utunzaji taarifa muhimu, kutuma na kupokea fedha pamoja na biashara za mitandaoni.
Dkt. Samia amesema kuwa mkongo huu kutatoa fursa kwa mitandao ya simu na watoa huduma wengine kuchagua mkongo wanaotaka kutumia na kuongeza ubora na kushusha gharama za intaneti.
“Misingi imara kwenye TEHAMA na mifumo ya mawasiliano kisera, kisheria na kitaasisi itawezesha kujenga uchumi jumuishi wa kidijitali (Digital Inclusive Economy) na kuinua maisha ya wananchi mijini na vijijini” amesema Dkt. Samia.
Amesema kuwa mradi huo unakwenda kuleta mapinduzi makubwa katika teknolojia pamoja na kuendelea kuweka msingi imara ya kisera pamoja na taarifa.
Amebainisha kuwa itawezesha kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika utoaji wa mawasiliano pamoja na kupunguza gharama za huduma ya internet.
“Naomba kuwe na huduma ya internet katika kwa wafanyabiashara (wamachinga) ili waweze kufanya mawasiliano yenye kuleta na kuwasaidia katika kufanikisha shughuli zao za kiuchumi” amesema Dkt. Samia.
Hata hivyo Rais Dkt. Samia ameiagiza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha anasimamia mifumo yote ya TEHAMA inasomana na taasisi zinazosimamia sera.
“Tufanye tathmini ili tutumie mfumo mmoja ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika Wizara” amesema Dkt. Samia.
Pia amesema kuwa Serikali imeanza mradi wa ujenzi wa minara mipya 758 kwa ajili ya kupanua wigo wa mawasiliano (coverage) itakayowanufaisha watanzania zaidi ya milioni 8 nchini na kupunguza gharama za kuweka mkongo kwenye hifadhi za barabara.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuwa teknolojia ya 5G inakwenda kufanya vizuri na kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa nchini, huku akieleza kuwa Serikali inaendelea kuwakaribisha wawekezaji.
Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika Dkt. Olusegun Ogunsanya, amesema kuwa wataendelea kufanya uwekezaji katika sekta ya mawasiliano ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo umetokana matokeo maagizo ya Rais Dkt. samia katika sekta ya mawasiliano.
Mhe. Nnauye amesema kuwa utasaidia kukuza uwekezaji pamoja na kufungua fursa za ajili nchini.
“Tutaweka free WiFi maeneo ya kumpuzikia, kwa wamachinga pamoja na vituo vya Mabasi Yaendayo Haraka” amesema Mhe. Nnauye.
Mhe. Nnauye ameeleza kuwa Rais ameendelea kufanya kazi kubwa na kuacha alama ambayo watanzania hawatakuja kusahau.