NA STEPHANO MANGO, SONGEA
KAIMU Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Gwisael Pagi amewataka Polisi Jamii Mkoani Ruvuma kufanya kazi kwa Weredi kwa kushirikiana na Wananchi ili kufichua na kudhibiti matukio ya kiuharifu katika jamii.
Hayo yamejiri katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Polisi jamii Mkoani Ruvuma yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea jana yaliyoshirikisha Jeshi la Polisi, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kimila, pamoja na viongozi wa Serikali za Mitaa kwa lengo la kutoa elimu ya ushirikishwaji katika masuala ya ulinzi shirikishi jamii.
ACP Pagi alisema mwaka 2006 kupitia waraka namba 3 wa Inspekta Jeneral wa Polisi nchini umeweka msisitizo katika suala la Polisi Jamii huku wakitambua kwamba Sheria za Polisi zinazungumzia Ushirikiano baina ya polisi na jamii na ndio maana Kauli mbiu yake hii; “Polisi jamii kwa maendeleo ya jamii ”
ACP Pagi alisema lengo la kukutana katika ukumbi huo ni kutekeleza mradi wa ukaguzi na Polisi kata katika kuzuia Uharifu ukiwa na malengo mahususi ya kusogeza huduma karibu na jamii ambao ulizinduliwa rasmi na Kamishina wa Polisi Faustin Chinogile mnamo tarehe 24 julai 2003 Mkoani Lindi kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa wa polis jamii nchini, ngazi ya Mkoa, Wilaya, na polisi kata pamoja na polisi jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia, ubakaji, Migogoro ya ardhi, Ushoga na matukio ya uharifu.
Akizungumza Msatahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema anaishukuru Serikali katika kusimamia suala la ulinzi shirikishi wameweza kupeleka Polisi kata kila kata ili kulinda usalama wa Raia na mali zao “alipongeza”
Mbano alisema Kwa upande wa Manispaa ya Songea suala la ulinzi shirikishi wamelipokea vizuri kwa kuwapokea Polisi kata kwa kila kata na kuwapa ushirikiano katika utendaji wa kazi zao za kila siku ikiwemo kutanzua baadhi ya changamoto ambazo hukwamisha utendaji wa kazi zao.
Ametoa rai kwa Serikali kuwawezesha Polisi kata kwa kuwapatia vitendea kazi kama Pikipiki ili kurahisisha utendaji wa kazi zao za kila siku ambapo pia amewataka Maafisa watendaji wa kata kutoa ushirikiano kwa Polisi kata hao kwa kuwsaidia Pikipiki pale wanapohitaji usafiri wawapo kituoni hapo kwani hivi karibuni Maafisa Watendaji kata wanatarajia kupewa Pikipiki kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi.
Kwa upande wake Kamisheni ya Polisi Jamii kutoka makao Makuu Dkt. Ezekiel Kyogo SP alisema “ siku ya leo ni mwendelezo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari kata pamoja na Viongozi wa Serikali za mitaa kwa lengo kwa kutoa elimu ya Farusafa ya jamii na ushiriki wa jamii katika mambo ya usalama pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia na kuwajenga polisi Kata waweze kuwa walimu katika jamii.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo walitoa shukrani kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataboresha utendaji wa kazi na kupunguza migogoro, na vitendo vya kikatili katika jamii.