Wafanyabiashara wa soko la Samaki la Kimataifa la mwaloni kirumba lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza wakiwa kwenye mgomo kutokana na kuongezewa kwa gharama ya kibali.
Bidhaa za Wafanyabiashara wa soko la Samaki la Kimataifa mwaloni kirumba zikiwa zimefungwa kutokana na mgomo.
…….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wafanyabiashara wa Soko la samaki la kimataifa la mwaloni lililopo katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza wamefanya mgomo wa kuendelea na shughuli zao za uzalishaji kutokana na kuongezeka kwa tozo ya ushuru wa kibari kutoka shilingi 10 mpaka 100 kwa kilo moja Mgomo huo umefanyika leo Alhamisi Agosti 10, 2023 katika soko hilo.
Wakizungumzia suala hilo wafanyabiashara hao wamesema wameshangazwa na kupanda kwa pesa ya kibali hali ambayo imeongeza gharama kubwa kwa gari moja yenye tani 15 huku wakiiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa uharaka kwani kwasasa hawafanyi shughuli yeyote mpaka muafaka utakapo patikana.
“Serikali iangalie suala hili kwamakini ili tuweze kufanya kazi zetu kwa amani,ongezeko la gharama ya kibali hiyo ni kubwa sana ukilingaisha na hali ya uchumi ilivyongumu kwa sasa”, wamesema.
Katika hatua nyingine Wafanyabiashara hao wamelalamikia suala la wafanyabiashara wakigeni kufika visiwani na kununua samaki ambapo wanapaswa kuishia kwenye soko hilo.
“Sisi tunatakiwa kwenda visiwani kuchukua Samaki na kuzileta kwenye soko kwaajili ya kuwauzia Wafanyabiashara wa kigeni lakini wao wamekuwa wakienda moja kwamoja visiwani na kununua samaki Hali ambayo imekuwa ikizolotesha biashara kwa wazawa”, wamesema Wafanyabiashara.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Kiomoni Kibamba amewaomba kuwa na subra kwani suala hilo limeshafikishwa kwenye ngazi za juu na linafanyiwa kazi.