Askofu wa jimbo kuu katoliki la Arusha,Usack Amani akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Respige Kimati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha katika uzinduzi huo
…………………………..
Julieth Laizer, Arusha
Arusha .Taasisi za kifedha zimeshauriwa kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi ili kuachana na mikopo umiza ambayo imekuwa ikiwarudisha nyuma kimaendeleo wananchi,katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Askofu wa jimbo kuu katoliki la Arusha,Isack Amani ameyasema hayo jijini Arusha katika uzinduzi wa Taasisi ya fedha ya benki ya Mkombozi ambapo amesisitiza benki kuu ya Tanzania kusimamia hilo ili kupunguza changamoto ya wananchi kushuka kiuchumi kupitia mikopo umiza.
Askofu Amani amewataka wananchi kuwa macho na kuepuka kuingia kichwa kichwa kwenye taasisi za fedha zinazotoa ushawishi wa haraka haraka ,ambazo hazieleweki zinazotoa mikopo inayokausha na mwishowe kuishia kupata hasara .
“Jamii iwe makini, hivi sasa wanatokea watu wanafungua vibenki vya ajabu ajabu kudanganya watu wachukue mikopo, na baadaye wanaishiwa kutapeliwa “amesema.
Ameitaka benki kuu ya Tanzania (BOT)ambao ndio msimamizi mkuu wa taasisi mbalimbali za fedha nchini , kuhakikisha usalama wa fedha katika sekta ndogo unazingatiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Respige Kimati, amesema sekta hiyo ya fedha imejipanua kutoa huduma bora kwa wananchi wake ikiwa ni mojawapo ya mikakati iliyojiwekea kuhakikisha wanawafikia wananchi ambao hawajafikiwa kwa kuongeza matawi zaidi ya kidigitali.
Amesema kuwa benki hiyo ina jumla ya mawakala mia saba huku kwa Arusha wakiwa na mawakala 20 pekee huku malengo makuu ikiwa ni kuwafikia wateja popote walipo na kuweza kupat huduma bora za kifedha ambazo zimesajiliwa kisheria .
“Benki hii ni benki inayofanya kazi kwa uadilifu mkubwa na inalenga kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa kati na wa wakubwa huku ikilenga kuwafikia wote wenye mahitaji sambamba na kutatua changamoto ambazo wajasiriamali wanakabiliana nazo.”amesema Kamati.
Mmoja wa Wateja katika benki hiyo, Adolf Olomi ameiomba taasisi hiyo iweze kutoa elimu juu ya mkopo ili wananchi waweze kujikwamua kiuchumi na kuweza kukuza biashara zao na kuondokana na changamoto mbalimbali.
“sisi tumefurahia sana ujio wa benki kama hii kwani inawapa fursa wafanyabiashara mbalimbali kuchangamkia na kuchagua benki kulingana na huduma zinazotolewa”amesema Olomi.
Hata hivyo amewataka Wafanyabiashara kuunga mkono kwa kufungua akaunti na kuchukua mikopo kupitia taasisi ili iweze kuharakisha biashara zetu.
Aidha amezitaka benki mbalimbali , kupunguza riba na kutoza riba ambazo kila mmoja anaweza kukopa kwani kuna benki ambazo zinatoza riba kubwa kuanzia asilimia 21 hadi 22 kwani hiyo ni kubwa sana hivyo kuwataka watoze asilimia 17 hadi 18 kwani ndo riba ambayo ipo sawa kwa wafanyabiashara .
Aidha amewataka wafanyabiashara kunufaika na benki hizo wafanyabiashara wajifunze kukopa na kuweka ili kujiendeleza kiuchumi .pia kupitia
Naye Mkurugenzi wa St Patrick ,Dina Mosha amesema kuwa,uwepo wa benki hiyo ni fursa kubwa hususani tunapokuwa na benki nyingi huku akiwataka kuangalia fursa ambazo zipo tofauti na benki zingine ikiwemo za wajasiriamali, na vijana huku wakiwasaidia vijana wa kiume zaidi kwani wengi wao wamekuwa wakikata tamaa kutokana na ukosefu wa mitaji hivyo waone namna ya kuwasaidia ili wasile mitaji,pamoja na kusaidia wakina mama kupata mikopo ya riba nafuu pia.
Aidha ameitaka benki hiyo kufungua bima kwa ajili ya Wazee wastaafu ambayo itawasaidia kwenda kutibiwa kote duniani kwani wengi waliostaafu huwa wanatengwa sana kwani wastaafu wengi wamekuwa wakipoteza maisha baada ya kustaafu .