Miili ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya ikiwa katika maandalizi ya Ibada ya Mazishi yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (kushoto), Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Prof. Cyriacus Binamungu wakiwasili katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki ibada ya mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akiwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (wa wa tatu kutoka kulia) katika ibada ya mazishi ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya katika ibada ya Mazishi yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akiaga miili ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya katika ibada ya Mazishi yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akiaga miili ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya katika ibada ya Mazishi yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Prof. Cyriacus Binamungu akiaga miili ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya katika ibada ya Mazishi yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa katika ibada ya mazishi ya ndugu watatu wa familia moja akiwemo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya yaliofanyika leo Agosti 8, 2023 katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam.
Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakiweka shada la mauwa katika Kaburi la aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho Dkt. Norah Msuya katika mazishi yaliofanyika leo tarehe 8/8/2023 katika Makaburi yaUnunio kwa Kondo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakishirikiana na ndugu kuingiza mwili wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho Dkt. Norah Msuya kaburini kwa ajili ya mazishi ambayo yamefanyika leo tarehe 8/8/2023 katika Makaburi ya Ununio kwa Kondo Jijini Dar es Salaam
Wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wakibeba na mwili wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho Dkt. Norah Msuya wakiwa wanaelekea makaburi kaburini ya Ununio Jijini Dar es Salaam.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani ameguswa na msiba wa Wanafamilia watatu akiwemo aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Norah Msuya, kwani Taifa limewapoteza watu muhimu, huku akitoa maagizo
kwa uongozi wa Hospitali Taifa ya Muhimbili kutoa huduma ya matibabu bure kwa wazazi wa marehemu.
Akizungumza leo Agosti 8,2023 katika hafla ya kuaga miili ya Marehemu Sia Msuya, Diana Msuya pamoja Dkt. Norah Msuya yaliofanyika katika Viwanja vya Lugalo Golf, Kawe Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameguswa msiba huo kutokana Marehemu walikuwa bado wanaitajika katika Taifa.
“Rais Dkt. Samia yupo pamoja na sisi, ametoa pole kwa wafiwa wote, ameniambia ameumizwa sana baada ya kuona wanawake wasomi ambao wanategemewa wanapoteza maisha” amesema Mhe. Chalamila.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha, amesema Chuo kitaendelea kumuenzi Marehemu Dkt. Norah Msuya kwa utendaji bora wa kazi kwani ameacha alama kubwa.
Prof. Mwegoha amesema kuwa Marehemu alikuwa mfatiliaji na kusimamia vizuri katika utekelezaji wa majukumu ya kitaalamu katika Kitivo cha Sheria Ndaki ya Dar es Salaam.
“Mchango wake ni mkubwa tutaendelea kumkumbuka katika maisha yake hapa duniani, amefanya kazi kubwa, ni mtendaji bora katika kipindi chote, ni mzalendo.”amesema Prof. Mwegoha.
Amesema kuwa Dkt. Msuya ameondoka akiwa mwenye nguvu na nafasi kubwa katika kutumia taaluma yake kwa manufaa ya Taifa kwani alikuwa zaidi ya Mwanasheria.
Amewashukuru wote waliofika kwa ajili ya kuwafariji wafiwa pamoja na kufanikisha siku hiyo muhimu ya mazishi ya Dkt. Msuya.
Marehemu Dkt. Norah Msuya akiwa ndugu zake walipata ajali ya gari siku Jumatano Agosti 2, 2023 katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutuma imesema kuwa ajali hiyo ikihusisha gari aina ya Toyota Prado na Scania.
Miili ya wanafamilia hao watatu Sia Msuya, Dkt. Norah Msuya na Diana Msuya, waliopoteza maisha katika ajali hiyo ya gari wakiwa safarini kuelekea msibani wilayani Same, miili yao imepumzishwa leo Agosti 8, 2023 katika Makaburi ya Ununio kwa Kondo baada ya siku sita za maombolezo.