Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jenereta za kisasa kwenye Hospitali za Wilaya za Lushoto na Muheza.
Jenereta hizo zimekabidhiwa ikiwa sehemu ya maombi ya hospitali hizo kwa MSD zikiwa na lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.
Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Lushoto Dkt.Godfrey Andrew ameishukuru Serikali kwa hatua ya maboresho ya sekta ya afya na kueleza kuwa jenereta hilo litawezesha baadhi ya huduma kufanyika hata pale ambapo umeme wa kawaida umepata hitilafu.
Kwa upande wake Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza Nuru Kionywaki amesema huduma za MSD zimekuwa na uhakika kwani ni kipindi kifupi toka hospitali imeagiza jenereta hilo na sasa limekabidhiwa.