Watumishi Housing Investiment (WHI) imetoa Rai Kwa watumishi wa umma pamoja na wanachama wa mifuko ya hifachi ya jamii.wanaotaka nyumba kujitokeza kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mnlbeya ili waweze kupata maelekezo jinsi ya kupata nyumba kwenye miradi iliyopo mwanza, Dodoma,Morogoro na Dar es salaam., na pia kupata elimu juu ya uwekezaji kwenye mfuko wa uwekezaji wa pamoja unaoitwa mfuko wa Faida (Faida Fund).
Wito huo umetolewa Leo Agosti 6 kwenye viwanja vya John Mwakangale na Meneja Masoko na Mawasiliano Bw. Raphael Mwabuponde ambaye amesema lengo kubwa la kuwa kwenye maonyesho hayo ni kuwaelimisha wananchi kuhusu mifuko inayoendeshwa na WHI ambayo ni mfuko wa nyumba unaoitwa WHI REIT kwenye mfuko huu WHI wanajenga nyumba ambazo wanauziwa watumishi wa Umma, Diaspora pamoja na wanachama wa mfuko ya Hifadhi ya jamii lakini pia wanajenga majengo Kwa ajili ya taasisi za serikali.
Sambamba na huo mfuko wa nyumba pia WHI inaendesha mfuko wa uwekezaji wa pamoja Faida(Faida Fund) na lengo kubwa la mfuko huu likiwa ni kuongeza thamani ya Fedha ya muwekezaji au kukuza mtaji wa muwekezaji.
Walengwa wa mfuko huu wa Faida (Faida Fund) ni Wakulima,wafanyakazi wajasirimali,Bodaboda,mamalishe,wavuvi, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali,NGO,Vikoba,,Saccos pamoja na wanafunzi
“Kupitia mfuko huu napenda kusema kwamba mtu yeyote yule ambae anataka kujiunga kwa ajili ya kuongeza thamani ya pesa yake anaweza kujiunga Kwa kupiga *152*00# arafu namba 1 malipo 6 WHI pia ataenda Faida Fund ambapo atakutana na kipengele ambacho kinahusiana na kutengeneza akaunti yake binafsi na kufuata maelekeza mpaka mwisho. Baada ya hapo utapewa namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number) ambayo ndiyo itatumika siku zote katika kununua vipande au kufanya uwekezaji amesema Mwabuponde.
Amesema muwekezaji atakuwa na uwezo wa kuwekeza Kwa kutumia tawi lolote la Benki ya CRDB, Wakala wa CRDB,Tigo pesa na Mpesa lakini pia Kwa kutumia Sim Banking
Vilevile Bw. Mwabuponde ameainisha kuwa huu mfuko gharama zake za uendeshaji ni nafuu Kwa sababu unatumia mfumo wa malipo wa serikali GePG lakini pia hakuna gharama ya kujitoa au kuingia kwenye mfuko huu lakini pia mfuko huu unamuwezesha mtu yoyote kukopa kwenye taasisi yoyote ya fedha kama vile benki kwani uwekezaji wake ndio utakua dhamna yake ya mkopo huo”ameongeza Mwabuponde
Ameongeza kuwa WHI imeamua kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa wanafunzi na vijana wadogo ili kujenga uelewa zaidi kwa wanafunzi na vijana kwanza kuujua mfuko na “Faida Fund” na faida zake lakini pia kupandikiza elimu ya uwekezaji kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja na vilevile kutoa elimu kuhusu kununua nyumba kwa njia ya mikopo ya muda mrefu(mortgage loans) jambo ambalo tunadhani likikaa vizuri kwao litakuwa na faida kubwa kwa kizazi kijacho katika uwekezaji.