Ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suruhu Hassan katika sekta ya elimu wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto kwenye vyuo vya mafunzo ya ufundi ili waweze kujikwamua kiuchumi lakini kupunguza wimbi la vijana mtaani waliokosa ajira.
Wito huo umetolewa na Rais wa shirikisho la vyuo vikuu wa Chama Cha Mapinduzi Yunus Selemen kwenye mahafari ya chuo hiko amesema wazazi wanapaswa kuunga mkono juhudi za Rais Samia ili kuleta maendeleo chanya ya Kwa Taifa.
Amesema chuo hiko kinatekeleza ilani ya chama Cha mapinduzi hivyo jumuiya ya wazazi na jumuiya ya vijana wa chama hiko kupeleka vijana kwenda kujifunza ili kupunguza uhaligu mbalimbali unaofanywa na baadhi ya vijana mitaani.
“Jumuiya ya wazazi na jumuiya ya vijana CCNamnapaswa kuleta vijana kuja kujifunza kozi mbalimbali ili kupunguza wimbi la utumiaji wa madawa ya kulevya na ujambazi linalofanywa na kundi kubwa la vijana Kwa kukosa shughuli ya kufanya wakija kujifunza watapata ujuzi utakaowasaidia kujiajili”amesema Selemani
Wanafunzi walioagwa kwenye mahafari hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam walikua ni 260 wa kozi tofauti ikiwemo pamoja na uhudumu wa hotel,ushonaji, Tehama,upambaji na urembo na utalii.