Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Mohamed Besta na Mkandarasi SINOHYDRO Corporation Ltd alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III jiji la Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Mohamed Besta akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto KM 23.3, inayojengwa na Mkandarasi SINOHYDRO Corporation Ltd leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Usafiri wa Haraka wa Mabasi BRT III kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto KM 23.3 jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa barabara ya BRT III kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongolamboto KM 23.3 sehemu ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.
………
Na Sophia Kingimali
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameagiza Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuhakikisha mradi wa Barabara ya Mabasi yaendayo haraka BRT3 kutoka katikati ya Jiji hadi Gongo la Mboto unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa na kwa wakati.
Amesema hayo baada ya kufanya ziara katika mradi huo wenye urefu wa zaidi ya Kilomita 23.3 pamoja na Vituo mbalimbali vya abiria ambapo amempongeza Mkandarasi anayejenga kwa kasi anayoenda nayo licha ya kuchelewa kidogo.
“Nimpongeze mkandarasi Kwa hii Kasi anayoenda nayo amechelewa kuanza lakini anafanya kazi nzuri mnapaswa kumsimamia ili aweze kuikamilisha Kwa wakati”amesema Profesa Mbawara.
Aidha Profesa Mbawara amesema kuwa mkandarasi kaajili vijana 94 Kwa ajili ya kusaidia kwenye ujenzi huo wakifanya kazi usiku na mchana ili kurahisisha kazi na kumaliza kazi Kwa wakati.
Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi Frank Mbilinyi amesema mradi umefikia asilimia 12 na kwamba shughuli za Ujenzi zinaendelea kufanyika mchana na usiku huku akiahidi utakamilika kwa muda uliopangwa kutokana na umuhimu wa Barabara hiyo kwa Wananchi.
“Tunatambua umuhimu mkubwa wa barabara hii tunafanya kazi usiku na mchana ili kuikamilisha kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu wananchi”amesema Mbilinyi
Aidha Mbilinyi amesema mradi wa mbagala umechelewa Kwa asilimia mbili kutokana na sababu mbalimbali lakini unatarajiwa kukamilika mwezi wa wa kumi.
Amesema mpaka Sasa ni marekebisho madogo yaliyobaki ili kukabidhiwa ikiwemo taa na miundombinu ya vituo.
“Huu mradi umechelewa kweli Kwa asilimia mbili lakini mpaka kufikia mwezi wa kumi tutakua tumeukamilisha na kukabidhi Kwa ajili ya kuanza kazi sehemu zilizobaki ni ndogo ndogo. Ameongeza Mbilinyi
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu tawala wa Wilaya ya Temeke Nicodemas Tambo na Katibu tawala Charangwa Seleman wamesema Barabara hiyo inawatumiaji wengi hivyo wamesisitiza ikamilike Kwa wakati ili kuwapunguzia Wananchi kero.
Hii barabara inategemewa sana na Wananchi Kwa shughuli zao za kiuchumi na kijamii hivyo mradi huu unapaswa ukamilike Kwa wakati ili kuwapunguzia wananchi kero wanayokutana nayo Sasa”amesema Charangwa.
Hadi kukamilika kwa mradi huo unatarajia kugharimu shilingi bilioni 231.