Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambaye ni msomi shahada ya kwanza ya masuala ya maendeleo ya jamii Lightness Mwasano ambaye ni mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya akisuka mkeka katika banda la TASAF kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF ambaye ni msomi wa Shahada ya kwanza ya masuala ya maendeleo ya jamii Lightness Mwasano ambaye ni mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya akipanga mikeka yake katika banda la TASAF kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TASAF Makao Makuu, Zuhura Mdungi wa nne kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wenzake wa mfuko huo kwenye banda lao katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Picha ya pamoja na wanufaika wa TASAF.
…………………………………
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeendelea kuwasaidia watoto waliozaliwa katika kaya masikini kufikia ndoto zao.
Hayo yameelezwa na Lightness Mwasano Mkazi wa Kata ya Kalobe mtaa wa Majengo jijini Mbeya ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mfuko wa TASAF na mshiriki wa maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane kupitia banda la TASAF amesema kupitia mfuko huo umemsaidia kusoma shule mpaka kufikia ngazi shahada ya kwanza masuala ya Maendeleo ya jamii katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Amesema baba yake alifariki mwaka 2009 na mama kubaki mjane ambapo alikua na watoto watatu huku akiwa Hana kazi na aliwalea kwa kuuza mbogamboga.
Amesema mama yake alishindwa kumudu ghalama za kuwalea na kupata mahitaji muhimu ikiwemo ya shule kutokana na kutokuwa na kipato cha kuendesha maisha katika familia.
“Mama alienda kujieleza Kwa viongozi wa serikali ya mtaa hivyo walimshauri kujiunga na mfuko wa TASAF na kweli tulisaidiwa kusoma mpaka nilipomaliza elimu yangu ya sekondari kidato cha nne wakati nipo kidato cha tano mkoani Kigoma mama aliugua na kufariki”amesema Lightness
Amesema baada ya mama yake naye kufariki bado TASAF waliendelea kuwahudumia katika maswala mbalimbali yakiwemo ya kielimu na kijamii.
Aidha Lightness ameongeza kuwa ameweza kusoma mpaka kufikia chuo kikuu kwakuwa alipata mkopo wa asilimia 100 ambao pia uliwasaidia wadogo zake kwenye mahitaji yao ya Kila siku shuleni na nyumbani.
Amesema kupitia TASAF hata Sasa mdogo wake ambae yupo kidato Cha sita anaendelea kunufaika na mfuko huo huku akiamini ataweza kusoma na kupatiwa mkopo wa serikali kwa asilimia 100.
Hata hivyo amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusaidia wanyonge huku akitoa wito kwa kaya zisizoweza kujikimu na kusaidia watoto wao kupata elimu kwenda kujieleza kwenye serikali za mitaa ili waweze kuingizwa kwenye mfuko huo na kupata msaada na kutimiza ndoto zao.