Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarehe 07 Agosti 2023 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebe nchini Uganda.
Makamu wa Rais amewasili nchini Uganda ambapo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi 25 Wanachama Wazalishaji wa Zao la Kahawa.