Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akisalimiana na Deogratias Maneno Mkurugenzi huduma za Biashara wakati alipotembela katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akisalimiana na Bw. Albogast Kajungu Meneja WMA Mbeya wakati alipotembela katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane mkoani Mbeya katikati ni Deogratias Maneno Mkurugenzi huduma za Biashara WMA.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akitoa maagizo kwa Deogratias Maneno Mkurugenzi huduma za Biashara wakati alipotembela katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane mkoani Mbeya.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akipata maelezo kutoka kwa Deogratias Maneno Mkurugenzi huduma za Biashara WMA wakati alipotembela katika banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane mkoani Mbeya.
………………………………….
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) ameipongeza taasisi ya Wakala wa Vipimo kwa kuendelea kusimamia usahihi wa vipimo kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya Kilimo.
Pamoja na pongezi hizo Mhe. Kigahe amehimiza Wakala wa Vipimo kuendelea kuhamasisha wakulima kijiunga katika vikundi ama vyama vya Ushirika (AMCOS) ambapo itakuwa rahisi kwa Serikali kuwawezesha kuwa na mizani sahihi na iliyohakikiwa ili waweze kuuza mazao yao kwa kuzingatia uzito sahihi unaotakiwa kisheria ambao ni uzito usiozidi 100 kg na kuacha kufungasha na kusafirisha mazao kwa mtindo wa Lumbesa na kutotumia vipimo batili kama ndoo, Madebe na Kangomba wakati wa uuzaji wa mazao yao kwani vipimo hivyo vinawapunja na kuwanufaisha wanunuzi.
Mhe. Exaud Kigahe ameyasema hayo alipotembelea banda la Wakala wa Vipimo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya kwenye Viwanja vya John Mwakangale.
Akizungumza Mkurugenzi wa Biashara Wakala wa Vipimo Bw. Deogratias Maneno amemueleza Naibu waziri Mhe Exaud Kigahe (Mb) kuwa Wakala wa Vipimo ni wadau wakubwa kwenye maonesho ya kilimo kwa kuwa inashiriki kwenye mnyororo mzima wa thamani tangu mkulima anapoanza uzalishaji wa mazao mpaka anapofika katika uzalishaji.
Pia, Bw. Maneno ameeleza kuwa Wakala inaendelea na usimamizi wa vipimo kwenye ufungashaji wa mazao ili kutokomeza ufungashaji wa mazao kwa mfumo wa Lumbesa ambapo kaguzi mbalimbali zinafanyika ili kukabiliana na suala hilo na Wakala inatumia nafasi ya ushiriki wake kwenye maonesho ya Nane Nane kuwaelimisha Wakulima na kuwataka wafuate Sheria na taratibu ili waweze kuuza mazao kwa kutumia mizani na wafungashe na kusafirisha mazao kwa uzito usiozidi kilo mia moja (100 kg).
Mkurugenzi Maneno amemueleza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kuwa Wakala wa Vipimo inaendelea kuhimiza Halmashauri mbalimbali kuanzisha vituo maalumu vya mauzo (Buying Centers) ambazo zitasaidia wakulima kupeleka mzao yao na wanunuzi kununua katika vituo hivyo ambavyo vitakuwa na mizani sahihi iliyo hakikiwa na Wakala wa Vipimo ili kuhakikisha kunakuwa na biashara ya usawa bila Mkulima kupunjika ili waweze kupata stahiki zao kulingana na kiasi sahihi cha mazao wanayouza.
Kadhalika, Mkurugenzi maneno amemueleza Naibu waziri Kigahe kuwa Wakala wa Vipimo inaendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi kwenye vyama mbalimbali vya Uhirika vya Msingi (AMCOS) ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wakulima wa mazao ya kimkakati kama pamba, korosho, ufuta na kahawa ili waweze kutumia mizani wakati wa uuzaji wa mazao yao na mara baada ya kutoa elimu Wakala hufanya kaguzi mbalimbali za kushtukiza kwa lengo la kijiridhisha kama mizani inatumika kwa usahihi kama ilivyohakikiwa kabla ya kuanza kwa msimu.
Mmoja ya Wananchi aliyetembelea banda la Wakala wa Vipimo na kupata elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipimo Bw. Lupakisyo Mahenge mkazi wa Mafinga Mufindi amesema amajifunza mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kutambua namna sahihi za kuandika alama kwenye bidhaa zilizofungashwa pamoja na kufahamu namna ya kutambua kama mzani umekaguliwa na Wakala wa Vipimo kupitia taarifa zinazojazwa kwenye stika inayowekwa kwenye mizani ambayo inaonesha mwaka na mwezi ambao kipimo kimekaguliwa.