NJOMBE
Wakati serikali ikitangaza kupanda kwa bei ya mafuta hapo agosti 2 mwaka huu wadau mbalimbali pamoja na wanasiasa wamelalamikia hatua hiyo na kuitaja kuwa ni chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha na kisha kuitaka ruzuku iwekwe kwenye nishati hiyo ili kukabiliana na mlipuko wa bei.
Siku nne zilizopita EWURA ilipandisha bei ya mafuta kutoka bei ya shilingi elfu 2800 na kuwa elfu 3200 Njombe jambo ambalo limesababisha nauli kuongezeka kwenye vyombo vya moto pamoja na bei za bidhaa.
Katika mkutano wa hadhara wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema katika kijiji cha Ilembula wilaya ya wanging’ombe mwenyekiti wa chadema mkoa wa Njombe Rose Mayemba amesema kupanda kwa bei ya mafuta kunakwenda kuongeza ukali wa maisha kwakuwa watu wenye kipato cha chini watashindwa kumudu gharama za baadhi ya bidhaa ambazo bei zake zinaathiriwa moja kwa moja na kupanda za mafuta hivyo serikali inapaswa hali za wananchi na kisha kusikiliza kilio chao.
Akitoa ushauri wa kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta Rose Mayemba amesema serikali inapaswa kujikita katika uzalishaji badala ya Kuagiza nje bidhaa zinazoweza kuzalishwa nchini kikiwemo chuma ,Ngano,mchele na vitu vingine ili kuokoa mabilioni ya fedha zinazotumika kuagiza bidhaa nje ya nchi.
“Ripoti ya BOT Nov 2022 inaonyesha Tanzania imetumia dola bil 1.1 ambayo ni sawa na fedha ya kitanzania trilioni 2.3 kuagiza chuma nje ya nchi wakazi wilayani Ludewa kuna hazina ya chuma zaidi ya tani bilioni 2 jambo ambalo ni la kushangaza kwasababu tungezalisha chuma wenyewe tuokoa fedha hiyo,Alisema Mayemba”
Wakati Chadema ikitoa msimamo na ushauri wake kwa serikali kuhusu kupunguza matumizi ya fedha nyingi za Tanzania kuagiza bidhaa na malighafi nje ya nchi ili kudhibiti mlipuko wa bei ya mafuta na bidhaa nyingine ,Wakazi wa mkoa wa Njombe nao akiwemo Erick Erasto ambaye ni dereva bodaboda wanasema tangu bei ya mafuta ipande hali ya imezidi kuwa ngumu na kisha kuitaka serikali kuona namna ya kukabiliana nao ikiwa ni pamoja na kuweka ruzuku.
“Kwa sasa tunanunua mafuta lita moja elfu 3200 kutoka elfu 2800 hapa Njombe jambo ambalo hata kwenye biashara yetu hailipi ,kwa hiyo tunaomba serikali iweke ruzuku kwasababu kila kitu kimepanda bei ,alisema Erick dereva” bodaboda.
Awali Rose Mbawala ambaye ni Mwenyekiti Bawacha Mbarali katika mkutano huo amewataka wananchi kuacha kuchagua kwa mazoea na badala yake wachagua mikakati inayotekelezeka ili kuletewa maendeleo kwasababu katika kipindi hiki cha miaka mitano wamejifunza jambo kubwa kwa mpango wa mungu.
Kwa Upande wake Katibu w Chadema NJOMBE Baraka Kivambe amezungumzia suala la kukithiri kwa michango ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika jamii ili hali ni jukumu la serikali na kisha kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa kuhoji.