Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe Leo Agosti 5,2023 kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kulia ni Bwana Aloyce Gervas, Mwakilishi wa Kurugenzi ya Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe na kushoto ni Dk. Nicholaus Tutuba Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Ushirikiano wa Viwanda wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mh. Misengo Pinda ametembelea Banda la Chuo Kikuu hicho kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kitaaluma na ubunifu.
Aidha amejulishwa kuhusu kampeni ya ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike Ndaki ya Mbeya na ameahidi kushiriki.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akizungumza jambo na Dk. Nicholaus Tutuba Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Ushirikiano wa Viwanda wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea Katika banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Jijini Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akiangalia Bidhaa mbalimbali katika banda hilo., kushoto ni Dk. Nicholaus Tutuba Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ubunifu, Ujasiriamali na Ushirikiano wa Viwanda wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Rais Chakula na Kilimo Mh. Peter Mizengo Pinda akipata maelezo Kutoka kwa Bi. Gloria Mushi, Afisa Masoko Chuo Kikuu Mzumbe.