Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi, Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo, Bw. James Ndege (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kutembelea Mabanda ya Taasisi mbalimbali za Seriakli, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya KIlimo Nanenane, yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale Jijii Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka (kushoto), akiagana na Bw. James Ndege, Afisa Mwandamizi, Elimu kwa Umma wa TNDA, Bw. James Ndege (kulia), mara baada ya kumaliza ziara yake katika Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeeya.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imeitaka jamii kutotumia dawa bila kufuata ushauri wa watalaam wa afya ili kulinda afya zao kwa kuwa matumizi holela ya dawa yanasababisha changamoto nyingi ikiwemo kusababisha usugu wa vimelea vya maradhi dhidi ya dawa sanjari na ini na figo kushindwa kufanya kazi jambo linaloweza kusababisha vifo au afya kudhoofika.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mwandamizi Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo, Bw. James Ndege wakati akielimisha makundi mbalimbali ya kijamii yaliyofika kupata elimu ya kazi za Taasisi hiyo kwenye banda la TMDA katika Maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Mamlaka hiyo inashiriki katika maonesho hayo ya kimataifa yanayofanyika jijini hapo kuanzia tarehe 1 – 8 Agosti, 2023 yakiwa na Kauli mbiu: “Vijana na Wanawake ni Msingi imara katika Upatikanaji Endelevu wa Chakula”.
“Bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi vilivyothibitishwa na TMDA ni muhimu katika kuokoa maisha ya watumiaji hata hivyo zikitumiwa bila kufuata ushauri wa wataalaam husika huweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya kama viungo vya mwili mfano figo na ini kushindwa kufanya kazi na wakati mwingine wagonjwa kupoteza maisha ama kuleta usugu wa vimelea kwa dawa zitakazotumiwa na jamii jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wananchi na taifa. Hivyo ni muhimu wananchi wanapopata changamoto ya kuugua wafike katika vituo vya kutolea huduma ya afya kwa ushauri na uchunguzi na kutumia dawa kama watakavyoelekezwa”, alisisitiza Bw. Ndege.