Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la EWURA, kupata taarifa za udhibiti wa huduma za nishati na maji, katika maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale, Mbeya, Agost 4, 2023.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Makete Bw. Willium Makufwe (kushoto) akipokea baadhi ya machapisho na ripoti mbalimbali za EWURA, kutoka kwa Bi. Edna Wilison, alipotembelea banda la EWURA, katika maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale, Mbeya.
Wananchi mbalimbali wakipata elimu kutoka kwa Maafisa wa EWURA walipotembelea katika Banda la Taasisi hiyo kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
………………………..
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa wananchi watembelee Banda la EWURA katika maonesho ya Nane Nane Mbeya.
Akuzungumza katika maonesho hayo Afisa Uhusiano wa EWURA Thobietha Makafu amesema kuwa katika majukumu yao wanadhibiti Nishati na Maji.
Amesema kuwa mafundi wa umeme wanatakiwa kusajiliwa ndipo waweze kufanya kandarasi za umeme katika nyumba na kufanya hivyo bila kuwa na leseni ya EWURA.
Thobietha amesema kuwa katika utoaji huduma EWURA inataka wananchi pale wanapoona kuna changamoto kwa watoa huduma wasisite kuwaambia ili kutatua changamoto hizo.
Amesema kuwa hata kwenye gesi wananchi wahakikishe kiwango gesi wanapata kulingana fedha zao walizolipa ‘Value for Money.
Tobietha amesema kuwa wameweka mfumo wa kusajili kwa wale wanaotaka kujisajili hawana sababu ya kusafiri kufuata huduma zao.