Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko akisalimiana na Afisa Kilimo wa Kampasi ya Mizengo Pinda ndugu Alfonsi Tambalu wakati alipotembelea katika Banda ilo Banda la Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda kilichopo mkoani Katavi, katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya, katikati ni Afisa Udaili Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda Ndugu Abel Lugimba.
Akitoa ufafanizi juu ya wanafunzi waliojisajili kwa kozi ya shahada ya Sayansi ya Usimamizi wa Rasilimali Nyuki Abel amesema usajili umefanyika kikamilifu ambapo mpaka sasa wamesajiliwa wanafinzi 192 na Stashahada ya uzalishaji na usimamizi wa mazao jumla waliomba 157.
Ameongeza kuwa kozi ya Astashahada ya uongozaji watalii na uwindaji wa kitalii wameomba wanafunzi 141.
Amefafanua kuwa jumla ya waombaji wote mpaka dirisha linafungwa wamefikia wanafunzi 490 ambapo kupitia maonesho ya Nanenane mpaka Jana dirisha linafungwa wameomba wanafunzi 50
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko akipata maelezo Kutoka kwa Afisa Udaili Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda Ndugu Abel Lugimba wakati alipotembelea banda hilo katikati ni Afisa Kilimo Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda mkoani Katavi Bw. Alfonsi Tambalu
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh. Mwanamvua Mrindoko akipokea zawadi ya mafuta ya kula mara baada ya kutembelea Katika banda hilo
Afisa udaili Kampasi ya Mizengo Pinda Bw. Abel Lugimba akitoa ufafanuzi juu ya wanafunzi waliojisajili Kwa kozi mbalimbali ili kujiunga na chuo hicho kwa Mkuu wa mkoa wa K atavi Mwanamvua Mrindoko.