Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ( TFNC) Dkt. Germanya Leyna akizungumza leo tarehe 4/8/20223 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya waandishi wa habari.
Watoa mada wakifafanua jambo katika semina ya waandishi wa habari kuhusu masuala ya lishe.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina kuhusu masuala ya lishe.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imewajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini kuhusu masuala ya lishe ikiwemo umuhimu wa maziwa ya mama katika kumnyonyesha mtoto.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya TFNC katika kuungana na nchi nyingine Duniani katika wiki ya Unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani ambapo kwa mwaka huu yamebebwa na Kauli Mbiu isemayo “SAIDIA UNYONYESHAJI: WEZESHA WAZAZI KULEA WATOTO NA KUFANYA KAZI ZAO KILA SIKU”
Akizungumza leo tarehe 4/8/20223 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ( TFNC) Dkt. Germanya Leyna, amesema kuwa kila mwaka Agosti 1-7 Tanzania inaungana na nchi nyengine kuadhimisho wiki ya
wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama Duniani kwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya lishe.
Dkt. Leyna amesema kuwa kupitia semina waandishi wa habari wapata elimu ya unyonyeshaji jambo ambalo ni rafiki katika kuhakikisha jamii inakuwa na uwelewa mkubwa.
“Lengo ni kutengeneza mazingira wezeshi kwa wakinamama ili waweze kutekeleza majukumu yao ya Taifa pamoja kupata nafasi ya kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama” amesema Dkt. Leyna.
Amesema kuwa afya ya mama mjamzito ni muhimu sana hivyo anategemea maarifa na elimu ambayo wameipata waandishi wa habari watafikisha kwa watanzania.
Amefafanua kuwa maziwa ya mama yana kiini kinga ambayo yanalinda kiini cha mtoto hasipate madhara pamoja na kuuwa chembechembe za wadudu,
“Maziwa ya mama yana protini, wanga ambayo yanaweza kumtosheleza mtoto kutokana na uhitaji wake” amesema
Dkt. Leyna.
Dkt. Leyna amesema kuwa serikali imeweka mazingira wezeshe kupitia sheria ya kazi na mahusiano, kanuni za kutangaza maziwa mbadala pamoja na kutoa rikizo ya uzazi kwa ajili ya baba na mama.
Hata hivyo amesema kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa baadhi ya sheria ikiwemo kuweka mazingira rasmi ya kazi kwa kupatikana chumba cha faraga kwa ajili ya mama kuweza kumnyonyosha mtoto maziwa.
“Tumekuja kukumbusha kuna sheria na kanuni ambazo zinamlinda mtoto na mama ambapo kwa pamoja tunaweza kuangalia namna ya kuwalinda ili kila mmoja anapata haki yake” amesema Dkt. Leyna.
Dkt. Leyna amesisitiza umuhimu wa lishe bora ili kuleta tija kwa Taifa katika kuhakikisha jamii inazingatia utaratibu na kuacha masuala ambayo sio rafiki katika ulaji kwa kuacha mazoezi ya tabia yanayotokana na Mila na desturi.