MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amezindua jengo la ghorofa 12 kwaajili ya Makazi na Biashara lenye vitasa janja “smart locks ” zitakavyowabana wapangaji wasiolipa kodi kwa wakati kushindwa kufungua milango yao pale watakapodaiwa.
Akizungumza katika ufunguzi wa jengo hilo la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)lenye vitasa vya kisasa “smart locks ” zinazowabana wapangaji wasiolipa kodi ,Dk,Mpango amesema Tanzania inaupungufu wa nyumba zaidi ya milioni 3 nchini hivyo kukamilika kwa jengo hilo, inapunguza upungufu huo.
Amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuweka mazingira wezeshi kwa TBA ili ijiendeshe yenyewe na kupunguza utegemezi kwa serikali na kwa hatua hiyo ya ukamilishaji wa jengo hilo la ghorofa 12 lenye uwezo wa kubeba familia 12 ,utasaidia upunguzaji wa ruzuku za serikali na kujitegemea.
Ameagiza sekta binafsi kushirikiana na TBA katika ujenzi wa nyumba ikiwemo TBA kujenga ghorofa maeneo yaliyorejeshwa serikali,ili kuondokana na changamoto ya makazi nchini.
Amesema mradi huo umezingatia ubunifu,ikiwemo wataalam waliohitimu vyuo vya ndani kwaajili ya kuwapatia uzoefu na ujuzi kwa vitendo na kupongeza uwekaji wa mfumo wa vitasa janja ambao utakuwa ni suluhisho ya ulipaji wa kodi za pango kwa wale wasumbufu
“Mradi huu umechochea uzalishaji katika viwanda wa vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa vya saruji,bati na kuongeza mapato kwa wazazwa wanatozalisha vifaa hivi,”amesema.
Kwamujibu wa Dk. Mpango, hivi sasa inafanya Tathimini kwa mashirika na Taasisi za umma zisizozalisha ili kuyafuta kuyafuta.
“Nawapongeza nyie TBA mpo kwenye njia sahibi ya kuondoka kwenye utegemezi wa ruzuku ya serikali kwani sasa mtaingiza mapato kupitia majengo haya ya biashara mnayojenga na wenginr waige mfano huu ili waondokane na mkono wa chuma wa kuja kuyafuta,”amesema.
Amewaagiza wapangaji wa nyumba hizo kutunza mazingira na wapangaji kuzingatia masharti ya mikataba ikiwemo ulipaji wa kodi kwa wakati ili kuondokana na adha ya kufungiwa milango hiyo ya vitasa janja.
Kadhalika, ameagiza TBA itunze mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yote wanayojenga nyumba ikiwemo kukidhi mahitaji ya soko na kuvuna maji ya mvua ili kumwagilia miti na maua yaliyopo kwenye majengo yao.
Kuhusu agizo la usafi alilotoa kwa Mkuu wa Mkoa na wakuu wake wa wilaya, alisema aliposhuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) amesikitishwa kuona wingi wa chupa zizliotupwa kwenye barabara nzuri ya kisasa ya njia nne.
“Hali hii haipendezi wananchi tunzeni usafi kwani Arusha kioo cha utalii na hususani sasa ambapo watalii wanamiminika baada ya Filamu ya The Royal Tour.
“Hali hii hairidhishi nakuagiza mkuu wa mkoa na wakuu wako wa wilaya shirikianeni kuhakikisha barabara hiyo na maeneo megine yanafanyiwa usafi na kuyalinda ili watu wasiendelee kutupa chupa,”alisema
Akitoa taarifa ya mradi wa jengo la Makazi la kibiashara lililopo katikati ya ya barabara ya Kinana na Afrika Mashariki eneo la Sekei Jijini Arusha,Msanifu wa jengo hilo ,Daud Kondoro ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) alisema chimbuko la mradi huo ni kuwezesha TBA kujikwamua kiuchumi na mapato yatakayowasaidia kuondokana na utegenezi kwa serikali Kuu.
Alisemaa mradi umetekelezwa kwa zaidi ya Sh.bilioni 6.665 na umetekelezwa kwa awamu nne hadi kukamilika kwake kutoka mwaka 2007 hadi 2023.
“Katika jengo hili la kisasa, linasakafu 12 na litachukua familia ya watu 22, ambapo kuna vyumba vitatu vya kulala,jiko sebule,vyoo na tumeweka vifaa janja yaani “smart locks” kwaajili ya wale wasiolipa kodi watashindwa fungua mlango kila mtu anapodaiwa hii itasaidia kuhimoza wapangaji kulipa kodi kwa wakati,”Alisema.
Aisha alisema wanatarajia kukusaya Sh.milioni 210 kila mwaka na mapato hayo yatawawezesha kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Prof. Makamo Mbarawa alisema ujenzi huo wa ghorofa umezingatia ubunifu ikiwemo uendelezaji wa ujenzi wa nyumba, katika maeneo mbalimbali nchini na kupitia utekelezaji huo
utawezesha wakala kujenga majengo kujenga nyumba nyingi za watumishi wa umma .
Alisema wameweka mfumo huo wa vitasa janja kwaajili ya kudhibiti kodi ya pango na kuhimiza watu kulipa kwa wakati ili kuondokana na kufungiwa milango.
Naye Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angelina Mabula alisema katika sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 imeonyesha ongezeko la watu lisiloenda sambaba na makazi ya watu huku mahitaji ya nyumba kwa mwaka ni 390,981 huku nyumba 2000 zikiwa zinahitajika lakini nyumba 1153 sawa na asilimia 0.02 pekee ndio zinajegwa
Alisema taasisi za sekta ya milki wanajenga nyumba zisizozidi 3000 na maghorofa ni 68,000 pekee huku uhitaji ukiwa mkubwa zaidi lakini majengo yanayojengwa hayajengwi maegesho.
“Sekta ya nyumba tunahitaji kusimamia ujenzi wa maegesho ya magari lakini watu wanaongezeka ila nyumba ni ndogo hivyo tutawezesha sekta binafsi kujenga nyumba za kisasa kwa bei nafuu”
Lakini pia wizara hiyo itaoa kibali cha kujenga nyumba kwa raia wa nje kwakibali maalum ili wanapoondoka wataziacha nyumba hizo na alitoa rai kwa waendeleza milki kujenga majengo ya kwenda juu badala ya majengo mtawanyiko ili kuondokana na kasi ya uendelezaji makazi.
Alihimoza wakala wa majengo kuendelea kujenga kwa kuweka tenkolojia ya smart lock ili kudhibiti wasiolipa kodi nchini.
Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu,Ally Jumbe aliwapongeza TBA kwa kujenga jengo hilo huku Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma,Vuma a,, Alisema mradi huo unatija kubwa kwa taifa kwani kunamiradi mingine inajengwa mbali na hakuna mahitaji muhimu ya kijamii ikiwemo ukosefu wa miundombinu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema chini ya uongozi wa Rais Samia Hassan Suluhu umechangia maendeleo ya Taifa ikiwemo Mkoa wa Arusha ikiwemo hili la uwekezaji kupitia TBA kwani licha jengo hili kuleta mandhari nzuri kwa Jiji la Arusha.