Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya siku moja ya Polisi Jamii.
Kamishna wa kamisheni ya Polisi Jamii Faustine Shilogile.
Wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla, amewataka wakaguzi wasaidizi wa jeshi la Polisi walioko kwenye kata kufanya kazi kwa weledi pasipo kumuonea mtu sanjari na kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi.
Makalla ametoa rai hiyo Jana Agosti 2, 2023 wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya polisi jamii yaliyofanyika Jijini hapa yakiwa na lengo la kuongeza ushirikiano baina ya wananchi na jeshi la polisi katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Amesema kuwa Kwa kushirikiana na watendaji na wenyeviti wa mitaa na vijiji kutaweza kuimalisha usalama na amani hatua ikayochochea maendeleo kupatikana kwenye sekta mbalimbali.
Kamishina wa kamisheni ya polisi jamii Faustine Shilogile ameeleza kuwa watendaji waendelee kutoa ushirikiano lengo ni kuhakikisha ushirikiano unakuwepo kwa wananchi na wanaendelea kuwa salama pamoja na Mali zao.
“Tuliamua kuanzisha zana hii ya polisi jamii Kwa kuwa polisi tuko wachache hatuwezi kuingia Kila sehemu ya Nchi yetu” alisema Faustine.
Faustine ameeleza kuwa hakuna mradi wowote unaweza kuanzishwa ukawa hauko kwenye eneo la kata ili kuendelea kulindwa na kuwa salama.
“Kama uko kwenye kata inamaana Kuna askari kata anaelinda, linapotokea lolote lile ni lazima tumuulize askari kata na mtendaji wa eneo hilo imekuwaje tukio hilo likatokea” alisema Faustine.
Kwa upande wake Kamishina msaidizi wa Jeshi la polisi Mstaafu Engelbert Kiondo amesema kuwa jeshi hilo tangu mwaka 60 baada ya uhuru limekuwa likifata taratibu za wazungu Kwa muda mrefu kazi ilifanyika mpaka miaka ya 2000 upolisi ulifanyika Kwa maagizo na sheria tu bila kujali masilahi ya wananchi.
“Polisi inajukumu la kufanya jamii iwe salama na kuwa na maendeleo endelevu, na sio kazi ya kupiga virungu kutishia watu na kuwapiga mabomu”amesema Kiondo.