Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
Na Ahmed Mahmoud
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameeleza kwamba Serikali ipo teyari kuhakikisha inashirikiana na kampuni ya kutotolesha vifaranga vya kuku kwenye Program ya BBT kuongeza thamani ya mnyororo wa mazao yake.
Ameyasema hayo Wakati akifungua kampuni ya Silverlands Wilayani Arumeru na kueleza kwamba kampuni hiyo imeweza kuunganisha huduma zake kwenye mradi wa BBT kukuza tasnia ya ufugaji kuku Kwa kuweka mtambo mkubwa wa kutotolesha vifaranga.
Aidha Waziri Ulega Amesema Serikali imekuwa na Mpango mkubwa wa chanjo Hivi karibuni watachanja ndege wafugwao nchini lengo likiwa ni kuweka mazingira mazuri ya kutambua ufugaji wenye tija na kuachana na ufugaji wa mazoea.
Kwa mujibu wa Waziri Ulega Serikali itaweka zuio la ungizaji wa vifaranga vya kuku iwapo nchi yetu itaacha kuzalisha vifaranga visivyo na ubora Kwa lengo la kuhakikisha tunazalisha vifaranga vitakavyouzwa hapa nchini na nje.
“Lakini tutambue kuwa magonjwa ya kuku Bado yapo hasa Kwa wale kuku wa kienyeji maarufu wa majumbani ndio maana tumekuja na Mpango wa chanjo utakaoshirikisha Serikali ngazi zote kuhamasisha chanjo hiyo”
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Silverlands Dkt.Ben Moshi Amesema kwamba kampuni hiyo itashirikiana na Serikali kwenye mradi wa vijana BBT na zaidi ya wafugaji 150,000 watanufaika na mradi huu kuboresha maisha yao.
Amesema tunaiomba Serikali tushirikiane nayo kuunganisha kuendeleza ufugaji kilimo kwenye mradi huu BBT. ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kuendeleza vijana .
Uwekezaji huu uchukuwa muda Kutoa Matunda lakini ni muhimu kujenga msingi imara na endelevu katika sekta ya mifugo tunaiomba Serikali idhibiti njia za panya za uingizaji wa mazao ya vifaranga
Tasnia ya ufugaji inaendeleza Mapinduzi ya kilimo na sisi Silverlands tunafura kuwa sehemu ya uwekezaji wakubwa kutekeleza lengo la Serikali katika tasnia hii ya mifugo tukitambua umuhimu wa Kutoa huduma Kwa mfugaji kuhakikisha anapata vifaranga vyakula vya kuku anapata mafunzo jinsi ya kuhudumia kuku kitaalam kuongeza tija na kipato Kwa kutumia bidhaa za Silverlands.
“Hadi Sasa Silverlands imewekeza zaidi ya Dola za kimarekani Milion 47 katika kujenga kiwanda hichi na Dola za kimarekani Milion 49 za kujenga kiwanda cha vyakula vya kuku huku tukiwa na wafanyakazi wa kudumu 4013 nchini”
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela Amesema Mkoa wa Arusha utaendelea kuhamasisha uwekezaji na agenda ya Mkoa huu ni Mifugo na tunatambulika kuwa ni vinara wa ufugaji hivyo Silverlands tutawalinda Sababu tunajua tija yao tutaongeza thamani ya mifugo.