Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Maduhu Kazi ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Usalama wa Raia “Civil Protection ” Nchini Algeria Leo Julai 30, 2023
Naibu Katibu Mkuu Maduhu yupo Nchini Algeria kwa ziara ya kikazi na ametembelea Makao Makuu hayo na kupokelewa na Kanali Omar Ouzouir, ambaye alimkaribisha na kufanya mazungumzo naye.
Kanali Omar amefura sana kwa ujio huo wa Naibu Katibu Mkuu huyo “tumefurahi sana kwa ujio wenu hapa Algeria na tunayofuraha kubwa kuwapokea kwani sisi tunajivunia kuwa Waafrica hivyo mjisikie mpo nyumbani”
Aidha Kanali Omar amesema Idara yetu tupo tayari kujenga mahusiano na kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika sekta ya usalama wa raia kwenye mafunzo ya kuzima moto na uokoaji.
Nae Naibu Katibu Mkuu amemshukuru sana kwa mapokezi na ukarimu mkubwa ambao wameuonesha. Pia nimeona namna gani mmejikita vizuri katika kuwahudumia wananchi wa Algeria kwa kuokoa maisha na Mali zao.
“Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji tunaamini tuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwenu” amesema Naibu Katibu Mkuu Maduhu.
Pia amemueleza lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kulijengea uwezo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili liweze kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania katika kiwango cha kimataifa.
Ushirikiano huu utakuwa na manufaa makubwa sana kwetu kwani Maafisa na Asakri wetu wanaamini watapata fursa ya kujifunza mengi kupitia mahusiano haya.
Naibu Katibu Mkuu amewapongeza na kuwashuruku sana pamoja na kuahidi kudumisha ushirikiano huo baina ya Idara hizi mbili.