Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kuwataka wakulima kutumia teknolijia ya Ndege Nyuki katika umwagiliaji na unyunyiziaji wa dawa kwenye mazao ili kuongeza ufanisi na uzalishaji wa mazao.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Bw. Abdul Njaidi kulia Afisa Uhusiano Mwandamizi wa mfuko wa PSSSF wakati alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Enock Bwigane Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw.Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Bw. Abdul Njaidi kulia Afisa Uhusiano Mwandamizi wa mfuko wa PSSSF wakati alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule akizungumza na Bw. Abdul Njaidi kulia Afisa Uhusiano Mwandamizi wa mfuko wa PSSSF wakati alipotembelea kwenye banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
…………………………………..
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania TCAA imetoa Rai Kwa Wakulima kutumia Teknolojia katika kilimo ili hasa katika unyunyiziaji wa dawa na pembejeo kurahisisha na kuboresha shughuli zao katika kilimo na kuongeza ufanisi wa uzalishaji mazao.
Akizungumza katika Maonyesho ya Kimataifa ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya Meneja Masoko na Mawasiliano wa TCAA Bw. Yesaya Mwakifulefule amesema TCAA inatoa elimu Kwa Wakulima kutumia ndege nyuki (Drones)kwenye shughuli za shamba kama kupanda mbegu na kumwaga dawa ili kurahisisha shughuli za kilimo.
Amesema Teknolojia hiyo itasaidia wakulima kupunguza gharama na muda hivyo itaongeza kipato na kuinua uchumi wa mkulima na Taifa Kwa ujumla.
“TCAA tumeshiriki maonyesho haya ya Nanenane ili tutoe elimu Kwa mkulima jinsi ya kutumia Drones katika shughuli zao ikiwa ni sehemu ya kuboresha kilimo na kuwa Cha kisasa kuendana na teknolojia sisi hatuuzi hizi Drone Bali tunatoa elimu kuhusu matumizi wakulima wanapaswa kujua hii si Kwa ajili ya mashirika tu hata mtu mmoja mmoja anaweza kutumia.’amesema Mwakifulefule
Amesema TCAA Ina lengo la kusimamia na kuelimisha matumizi Kwani wao ndio wenye jukumu la kusimamia vyombo vya anga.
Sambamba na hayo Mwakifulefule ameongeza kuwa TCAA inatoa mafunzo ya kutumia Drones huku akisisitiza kuwa hairuhusiwi mtu kuendesha Ndege nyuki bila kibali kutoka Kwa mamlaka husika.
“Tuna chuo cheti Cha CTC Kuna mafunzo ya wiki nne jinsi ya kuopareti Drones na kupewa cheti hivyo wakulima waje Kwa wingi tuwape elimu jinsi ya kutumia Drones ili waboreshe kilimo Chao na kuongeza mapato”ameongeza Mwakifulefule
Amesema ni makosa kisheria kutumia Drones kwenye shughuli yeyote bila kuwa na leseni kutoka kwenye