Mkurugenzi wa Asasi ya Strategic Alternative Learning Techniques (SALT) Bi. Rebeca Hudson Lebi akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/8/2023 Jijini Dar es Salaam kuhusu matembezi hisani yanayotarajia kufanyika tarehe 24/9/2023 katika viwanja vya Farasi (The Green Osterbay).
Balozi wa Asasi ya Strategic Alternative Learning Techniques (SALT) Bw. Mustapha Musaa akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/8/2023 Jijini Dar es Salaam kuhusu matembezi hisani yanayotarajia kufanyika tarehe 24/9/2023 katika viwanja vya Farasi (The Green Osterbay).
Meneja wa Masoko Bw. Ally Mpita akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/8/2023 Jijini Dar es Salaam kuhusu matembezi hisani yanayotarajia kufanyika tarehe 24/9/2023 katika viwanja vya Farasi (The Green Osterbay).
Mfanya advocay kuhusu mambo ya watu wenye ulemavu Bi. Zena Akuwa.
Mazizi mwenye mtoto wa matatizo ya ufahamu Bibie Abdullah akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 2/8/2023 Jijini Dar es Salaam umuhimu matembezi hisani yanayotarajia kufanyika tarehe 24/9/2023 katika viwanja vya Farasi (The Green Osterbay) kwa ajili ujenzi wa Mabweni ya watoto.
Baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na watoto wenye matatizo ya ufahamu.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Asasi ya Strategic Alternative Learning Techniques (SALT) iliyoanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto na vijana wenye matatizo ya ufahamu inatarajia kufanya matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangisha shilingi 765,000,000 ili kukamilisha ujenzi wa awali ya Mabweni mawili (2), Viwanda vitano (5), Jengo la Utawala, Vyumba vya wasaidizi, Jengo la mazoezi tiba pamoja na Hall lakulia chakula.
Hatua hiyo imekuja baada ya Asasi ya
SALT kupokea idadi kubwa ya watoto wenye matatizo na kukosa sehemu ya kuwaweka, hivyo wameamua kuanzisha matembezi hisani yanayotarajia kufanyika tarehe 24/9/2023 katika viwanja vya Farasi (The Green Osterbay) kuanzia saa 12:30 asubuhi ambapo kutakuwa na kilometa 2.5 ya watoto pamoja na kilometa 5 na 10 kwa wakubwa ili kufungua fursa kwa wadau kuchangia.
Akizungumza leo tarehe 2/8/2023 na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Asasi ya SALT Bi. Rebeca Hudson Lebi, amesema kuwa fedha hizo wanatarajia kupata kutoka kwa wahisani pamoja na watanzania wenye mapenzi mema kwa kuchangia pamoja na kuuza T-shirt kwa Shillingi 35,000.
“Kauli mbiu yetu SALT : tunaona uwezo wako, tunakutia moyo na tunaenda pamoja kwenye mapinduzi ya viwanda” amesema Bi. Lebi.
Bi. Lebi amefafanua kuwa asasi ya Salt ilianzisha Chuo Cha Ufundi na uzalishaji kwa ajili ya kuwaandaa vijana wenye changamoto za ulemavu wa ufahamu kuweza kuzalisha bidhaa kuingiza kipato chake binafsi na Taifa kupitia mpango wa kuanzisha viwanda vidogo katika asasi hiyo.
Amesema mpaka sasa kuna watoto 83 wanapata mafunzo ya utengenezaji wa sabuni za kuogea, shampoo, mafuta ya kupaka, vitambaa vya batiki, shanga na hereni, mikate na cake, jam na pickles, siagi ya karanga, ufungaji wa samaki na kuku pamoja na bustani za mboga mboga.
“Kuna zaidi ya watoto 451 wenye matatizo ya ufahamu ambao wanapenda kupata mafunzo na huduma lakini nafasi ni ndogo tulionayo haitoshi” amesema Bi. Lebi.
Amesema tayari watoto wamefanikiwa kuzalisha bidhaa ikiwemo mafuta ya kupaka, shampoo ya kuongea, shampoo ya kuosha magari ambazo zimewekwa nembo ya milia (Barcode) na zipo kwenye kukamilisha nembo ya Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
“Watoto wenye matatizo ya ufahamu kwa kiasi kikubwa wameachwa na jamii kutoka baadhi ya watu bado wanaamini kupata mtoto mwenye ulemavu amepata hasara jambo ambalo sio kweli, naomba wadau mbalimbali tujitokeze kuwasaidia watoto wetu” amesema Bi. Lebi.