Na Sophia Kingimali
Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biteko amekutana na wadau na taasisi mbalimbali za madini kutoa na kupokea maoni ya marekebisho ya sheria na baadhi ya kanuni zake ili kuboresha mazingira ya biashara ya madini na kuvutia uwekezaji.
Hayo ameyasema Leo Agosti mosi jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupokea maoni ya marekebisho ya sheria za madini na kanuni zake Dkt .Biteko amesema ni suala la kukusanya maoni lilianza muda mrefu hivyo utoaji wa maoni hayo wupo hatua ya mwisho.
“Ni vema tukutane na wadau wetu kabla maoni haja sainiwa na Waziri mwenye dhamana kuwapa mrejesho wadau wetu kabla hazijaenda kusainiwa na kufanyiwa kazi lazima tukubaliane,”amesema Dkt. Biteko.
Amesema kwanza wajue hayo mambo wanayozungumza maoni yao yamezingatiwa kama hayakuzingatia tuwape sababu kwa nini.
Amesema wametenga siku moja kwa ajili ya kupitia hizo kanuni imani yao watatoka na kanuni ambazo ni bora zaidi ili ziweze kuwasaidia wafanyabiashara.
Dkt. Biteko akizungumzia kuhusu marekebisho ya kanuni amesema kanuni zipo nyingi kuna kanuni inahusiana na masoko ya madini na changamoto wanaziona zipo pale hasa kwenye maeneo ya adhabu.
Amesema kuna kanuni ya uongezaji thamani ya madini wameamua kuanzisha leseni ndogo za uchenjuaji madini hiyo mialo ambayo wanachenjua zamani ilikuwa watu wanafanya bila leseni.
Amesema wameanzisha leseni ndogo pia ilikuwa watu wanajenga mialo ya uchenjuaji mahali popote kwenye makazi ya watu wameamua kuweka mazingira mazuri zaidi na kusimamia.
Ameeleza kuwa kuna kanuni nyingine ushiriki wa nchi kwenye uchumi wa madini na yapo maeneo wachimbaji wakubwa wana yalalamikia wanapokwenda kwenye masoko ya kimataifa wanakosa mtaji kwa sababu ya vipengele.
Aidha amesema wanaangalia kwa pamoja waone ni kipengele gani ambacho watarekebisha ili kiweze kukidhi mahitaji ya wadau wao.
Amesema marekebisho mengine yapo kwenye sheria ambao utaratibu ni mrefu kidogo lazima wachukue maoni ya wadau ili yaweze kufanyiwa marekebisho.
“Hili jambo ni mchakato mara baada ya kupata maoni serikali na wizara ya madini kushirikiana na taasisi zingine muhimu na wadau wameshirikishwa kutoa maoni Yao Kwa hiyo kanuni itakayotungwa itakuwa shirikishi itakuwa inawahusu watu wanayoijua,” amesema.
Nae Mwenyekiti wa Chemba ya madini Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema kuwepo Kwa kongamano la maoni ni jambo muhimu sana kwa wadau wa madini ni fursa Kwani inatoa nafasi Kwa wadau kutoa maoni Yao yatakayoleta mabadiliko kwenye sheria.
“Changamoto zipo nyingi tuliwasilisha kwa Serikali kufanya Marekebisho ya kanuni ili kutoa fursa kwa wachimbaji, leo tumefanya awamu ya kwanza bado siku mbili tutaendelea kutoa mapendekezo,” amesema Mhandisi Rweyemamu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi ya Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), Tariq James amesema wanashukuru Rais Dk. Samia Suluhu kwa kuona wadau wanapaswa kushiriki kutoa maoni ya mabadiliko mbalimbali ya sheria katika sekta ya madini