RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) wakimsikiliza Dkt. Faki Ame Mkuu wa Uzalishaji wa Mifugo Idara ya Maendeleo ya Mifugo Zanzibar, akitowa maelezo ya Mmoja wa Ngombe wa maziwa, wakati akitembelea maoneso ya Kilimo Nanenane katika banda la Mifugo yanayofanyika katika viwanja vya Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 1-8-2023, baada ya kuyafungua.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa Wataalamu wa Kilimo, Idara ya Kilimo Zanzibar Ndg.Salum Rehani, akitowa maelezo ya Mlo bora kwa Siku ukiwa na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali vya Uwanga, wakati akitembelea banda hilo baada ya kuyafungua Maonesho ya Nanenane ya Kilimo 2023 katika viwanja vya Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi “A”Unguja leo 1-8-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsiliza Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar CP.Khamis Bakar Khamis, wakati akitembelea Shamba Darasa la Chuo cha Mafunzo Zanzibar katika viwanja vya Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja baada ya kuyafungua Maonesho ya Nanenane ya Kilimo Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja viwanja hivyo,baada ya kuyafungua leo 1-8-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Kilimo Umwagaliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akivuna miwa katika Shamba Darasa la Chuo cha Mafunzo Zanzibar, katika viwanja vya Maonesho ya Nanenane ya Kilimo Zanzibar Kizimbani Dole Wilaya ya Magharibi “A” Unguja baada ya kuyafungua maonesho hayo leo 1-8-2023 na (kulia kwa Rais) Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji,Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe.Shamata Shaame Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakipata maelezo ya ufugaji wa Samaki aina ya Sato kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Moh’d Makame Haji, akitowa maelezo wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane ya Kilimo Zanzibar, katika viwanja vya Kizimbano Dle Wilaya ya Magharibi “A” Unguja baada ya kuyafungua maonesho hayo leo 1-8-2023. Na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa.(Picha na Ikulu).