Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akizungumza wakati ufunguzi wa Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa ulifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Ndg. Juma Khatib akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa ulifanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini.
Msajili wa Vyama vya Saisa, Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Prof. Alexander Makulilo ambaye alikuwa mtoa mada kuhusu matumizi ya viongozi wa dini katika siasa, mavazi na vitendo vya walinzi wa vyama pamoja na matumizi ya lugha katika mikutano wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba akichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo tarehe 1 Agosti 2023.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe akichangia mada wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo tarehe 1 Agosti 2023. Mkutano huo maalumu umewashirikisha baadhi ya viongozi wa dini na wawakirishi kutoka katika Taasisi za kirai kwa lengo la kujadili namna bora ya utengamano baina ya siasa na dini nchini.
Msajili wa Vyama vya Saisa, Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe mara baada ya kumaliza Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo tarehe 1 Agosti 2023.
……………………………
Na Sophia Kingimali
Kutoka na mazingira mazuri yaliyowekwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siasa hapa nchini msajili wa vyama ametoa wito Kwa vyama vya siasa kufanya siasa zinazozingatia Sheria ili kuendelea kulinda amani utulivu na umoja wa kitaifa.
Hayo ameyasema Leo wakati wa mkutano wa Baraza la vyama vya siasa lililowakutanisha viongozi wa dini na vyama vya siasa lengo likiwa kuelimishana namna ya kufanya siasa safi zitakazolinda utu na Taifa Kwa ujumla.
Jaji Francis Mutungi amesema Baraza limekua likifuatilia mwenendo wa siasa zinazoendelea nchini hivyo wameona ipo haja ya kuwakutanisha wanasiasa na viongozi wa dini ili kuelimishina jinsi ya kufanya siasa Kwa kutenganisha kazi za siasa na kidini.
“Tumekutana Leo na viongozi wa dini na viongozi wa siasa Kwani tumekua tukifuatilia siasa zinazoendelea hapa nchini tumeona sio nzuri Kwani kumekuwa na matumizi ya lugha za matusi na kukejeli viongozi pia viongozi wa dini kuhusishwa kwenye siasa hizo.”amesema Mutungi
Amesema mazingira mazuri aliyoyaweka Rais Samia katika kufanya siasa yanapaswa yatumike vizuri ili kuboresha siasa nchini.
Ameongeza utulivu, amani na umoja wa kitaifa usipokuwepo hakutakua na siasa badala yake ni kuliingiza Taifa kwenye mpasuko.
Kwa upande wake muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Alexander Makulilo amesema uhusiano wa siasa na dini ni changamano hivyo serikali inapaswa kuweka Sheria ili kuratibu muungano huo.
Amesema Sheria zimekataza kutumia viongozi wa dini katika majukwaa ya siasa ili kunadi sera za vyama.
Aidha Makulilo ameongeza kuwa matumizi ya lugha za uchochezi,kuzalilisha nchi,lugha za kibaguzi,lugha za kuzalilisha jinsia na lugha za kuzalilisha nchi zimepigwa marufuku badala yake vyama vya siasa vinapaswa kuuza sera zao ili waungwe mkono.
Sambamba na hayo Makulilo ameongeza kuwa Sheria hairuhusu chama chochote Cha siasa kuwa na walinzi wa viongozi na Mali za chama badala yake kazi hiyo ni ya jeshi la polisi.
Kwa upande wake mwanasiasa mkongwe John Cheyo ametoa Rai Kwa wanasiasa nchini kuwa Wazalendo wa nchi Yao Kwa kufanya siasa zisizozalilisha nchi Wala kumtukana Raisi au kiongozi yeyote wa serikali na chama.
“Ni aibu aibu Kwa kiongozi wa siasa kusimama jukwaani na kuanza kuisema nchini yako na viongozi wako hiyo sio siasa ambayo inapaswa kuwepo huo sio uzalendo tunapaswa kuwa Wazalendo kwanza Kwa nchi yetu.”amesema Cheyo
Nae Padri Frolence Lutaiwa kutoka Baraza la Maaskofu TEC amesema viongozi wadini wanapaswa kukemea maovu na si kushiriki katika ouvu hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuwaasa wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu zenye kujenga umoja,amani na mshikamano wa Taifa
Nae mwenyekiti wa Jumuiya na taasisi za kiislam nchini shekh Musa Kundecha amesema ni ngumu kutenganisha dini na siasa hivyo viongozi wanapaswa kutumia majukwaa siasa kutangaza amani na Imani ili kufanya wananchi kuwa na hofu ya Mungu na si kuwabagua kutokana na uchama au udini.
Mkutano huu wa Baraza la vyama vya siasa uliowakutanisha viongozi wa dini unalengo la kujadili namna ya Bora ya kufanya siasa za kistaarabu Kwa kufuata Sheria na katiba ili kulinda maslahi ya nchi.