Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kutoka kwa Justine Seni Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023.
Dkt. Philip Mpango amelipongeza Shirika la Bima la NIC kwa kubuni bima ya Kilimo kwa ajili ya wakulima kwa sababu wakulima walikuwa kama wamesahaulika, hivyo ujio wa bima hiyo ni ukombozi kwa wakulima wa hapa nchini na kwamba itasaidia kuwa na uhakika wa shughuli zao za kilimo.
Awali akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amesema Wizara ya Kilimo ilianza programu ya bima ya Kilimo kwa kuanza na shirika la bima la NIC, baada ya bima hiyo kuonesha mafanikio sasa makampuni mengine ya bima pia yameanza kutoa huduma hiyo kwa wakulima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Kilimo Ndugu Hussein Bashe wakati alipowasili kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde wakati alipowasili kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023, Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mjumbe wa NEC Taifa CCM kutoka Mkoa wa Mbeya Bw. Richard Kasesela wakati alipowasili kwenye ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikata utepe kushiria ufunguzi wa maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023 pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika ufunguzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati alipotembelea banda la NIC katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023, wa pili kutoka kulia ni Justine Seni Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
Baadhi ya watumishi wa NIC wakiwa katika banda la shirika hilo katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maagizo kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na kupongeza Shirika la Bima la NIC wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023, wa pili kutoka kulia ni Justine Seni Meneja wa Shirika la Bima la NIC Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Efrancia Mawala Afisa Habari Mwandamisi NIC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiondoka katika banda la Shirika la Bima la NIC akiwa ameongoza na Spika wa Bunge Mh. Tulia Ackson na Waziri wa Kilimo Hueesin Bashe mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya leo Jumanne Agosti 1,2023.