Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Enosy Swalle amesema Serikali ya imeendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu hapa nchini ili kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa katika anapata haki msingi ya kupata elimu.
Swalle amesema hayo wakati akikahua ujenzi wa mradi wa shule ya sekondary Ikondo k ambapo amesema kuwa wanafunzi wa sekondary wamekuwa wakifuata elimu umbali mrefu katika kata jirani ya Ukalawa hivyo ili kumaliza changamoto hiyo serikali ikatoa fedha kiasi cha mil 500 ili kufanikisha ujenzi wa shule ya kata ya Ikondo.
Aidha mbunge huyo amewataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ili kuzalisha wasomi ambao ni wataalamu kutoka kada tofauti nchini
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ikondo Milius Lupenza amesema kuwa shule hiyo imeleta mapinduzi na kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali wa zaidi ya km 20 kufata elimu kata ya Ukalawa jambo ambalo liliongeza utoro na kuathiri kiwango cha taaluma.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondary Ikondo Mekraud Kyando amesema kuwa kusogezwa kwa huduma ya shule ya sekondari katika kata ya Ikondo kutaongeza idadi ya wahitimu wa kidato cha nne na kuendelea kwani watoto wengi walikuwa wakiishia njiani kwasababu ya kutembea umbali mrefu kutafuta elimu huku wanafunzi nao wakisema serikali imetambua changamoto kubwa ambayo ilikuwa inakwamisha ndoto zao kwa muda mrefu.