Asilimia kubwa ya wakazi wa vijiji vitatu vilivyopo katika kata ya Tae wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wametii agizo la serikali kutakiwa kuachana na Kilimo cha Mirungi, biashara haramu ya Dawa za kulevya kwa kufweka na kung’oa visiki vyote kwenye maeneo yao ya mashamba.
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni alitoa muda wa Mwezi mmoja kukamilisha zoezi hilo ambapo tangu Julai 10 mwaka 2023 ilipotolewa agizo hilo kumekua na mwitikio mkubwa wa watu wanaosafisha upya mashamba yao na kugeukia kilimo cha mazao mengine ya Chakula na biashara kama ilivyo elekezwa.
Miongoni mwao ni familia ya Justine Niarira ambao walikamatwa wakati wa Oparesheni iliyofanywa na serikali kukata Mirungi kwenye vijiji hivyo, ambao wanasema wameamua kuajiri vibarua wa kutoa visiki na kusafisha upya Shamba lao.
Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa Agizo hilo Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema asilimia kubwa ya wakazi wa Kijiji hicho wametii na wapo baadhi wanaotoa taarifa kufichu maeneo yalipo mashamba mengine ambapo kipindi cha Oparesheni hayakufikiwa.
“Tunacho kisubiri ni ule muda wa mwezi mmoja nilioelekeza wenye mashamba kuondoa wenyewe kwa hiari, muda huo ukiisha tutarudi tena kule kwaajili ya kuchukua hatua, tukakao wakuta tutakamata”.Alisema Mkuu wa wulaya ya Same.