Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (wa kwanza kulia), na Naibu Spika na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa pili kulia), kutembelea eneo la Jangwani ambapo Mradi mkubwa wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi, ikiwemo ujenzi wa daraja kubwa la juu la Jangwani, unatarajiwa kujengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mapema mwakani, kwa gharama ya zaidi ya dola za Marekani milioni 350. Lengo la mradi huo ni kukabiliana na mafuriko pamoja na kuimarisha mipango miji ya Jiji la Dar es Salaam. Ziara hiyo fupi imefanyika baada ya kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia, kilichofanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (wa pili kushoto), Naibu Spika na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deo Ndejembi (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete (wa nne kulia), wakimsikiliza kwa makini mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), akieleza kuhusu mradi wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani, unaotarajiwa kujengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia hivi mapema mwakani kwa gharama yad ola za Marekani milioni 350, kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi. Lengo la mradi huo ni kukabiliana na mafuriko pamoja na kuimarisha mipango miji. Ziara hiyo fupi imefanyika baada ya kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia, kilichofanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa saba kulia), Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deo Ndejembi (wa tisa kushoto), Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (wa sita kulia), Naibu Spika na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Azzan Zungu (wa nane kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete (wa tisa kulia), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, pamoja na wataalamu kutoka Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ziara fupi ya kutembelea eneo la jangwani ambapo, Mradi mkubwa wa uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi, ikiwemo ujenzi wa daraja kubwa la juu la Jangwani, utajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mapema mwakani, kwa gharama ya zaidi ya dola za marekani milioni 350. Lengo la mradi huo ni kukabiliana na mafuriko pamoja na kuimarisha mipango miji. Ziara hiyo fupi imefanyika baada ya kikao kati ya Serikali na Benki ya Dunia, kilichofanyika ofisi za Hazina Ndogo, Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF-Dar es Salaam).
……..