Na Sophia Kingimali
Takribami asilimia 65 za uzalishaji wa umeme nchini unategemea gesi hivyo Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC linatarajia kufanya marekebisho ya visima vya kuzalisha gesi kwenye kitalu cha Manzi Bay Mtwara Lingo ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Julia 28 jiini Dar es Salaam mMneja Uendeshaji na Uzalishaji wa Gesi Mhandisi Felix Nanguka amesema ukarabati wa visima ni kwa ajili ya kuendeleza gesi inayozalishwa nchini ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi.
“Tunatarajia kukarabati visima vilivyopo Mnazi Bay Mtwara ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi na kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini”amesema Nanguka
Aidha Nanguka amesema kuwa pamoja na ukarabati wa visima Mnazi Bay pia wanatarajia kuongeza uzalishaji wa kisima namba 1 KMD 1 ambacho kinatoa gesi kwa ajili ya umeme unaozalishwa mkoa wa Lindi na Mtwara na pia gesi inayoingia kwenye bomba kubwa linalopeleka gesi Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi ya Gridi ya taifa na viwanuada.
Amesema kwa sasa kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha takribani futi za ujazo milioni 11 kwa siku ambapo baada ya marekebisho kisima hico kitaongeza ujazo wa futi milioni 7 hivyo ufanisi wa kisima hicho utafikia asilimia 65.
“Kwa sasa uzalishaji wa umeme nchini ni zaidi ya asilimia 65 unategemea gesi inayozalishwa nchini hivyo zoezi hili ni muhimu kwani litasaidia ongezeko la mega wati 35 za umeme nchini”Ameongeza Nanguka
Aidha TPDC imeweka kwenye mipango yake kuongeza uzalishaji kwenye maeneo mengine ikiwa marekebisho ya visima vyote nchini ytakamilika pia uendelezaji wa gesi ambayo inatarajiwa kuanza kutumika 2025.