Na Sophia Kingimali
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Geogre Simbachawene ametoa rai Kwa watendaji wakuu wa wakala za serikali kujitathimini utendaji kazi wao kama umekidhi malengo ya uwazishwaji wake.
Hayo ameyasema Leo Julai 27,2023 wakati wa kikao Cha watendaji wakuu wa wakala za serikali chenye lengo la kujadili mambo mbalimbali kuhusu wakala hizo amesema lengo la uanzishwaji wa wakala hizo ni kuisaidia serikali katika utendaji kazi wake na kuhakikisha inachangia katika pato la Taifa.
“Kuna baadhi ya wakala zinafanya vizuri na Kuna nyingine zinafanya vibaya hivyo niwaombe wakala mjitathimini kama mmefikia malengo ya uwazishwaji wenu”amesema Simbachawene
Aidha amesema wakala zinapaswa kutumia mifumo ya Tehama katika utendaji wake ili kujenga utumishi mmoja.
Amesema wakala zinapaswa kushirikiana na wizara mama ili kujenga mifumo ili kuboresha utendaji.
“Hii mifumo inapaswa iwe shirikishi ili kurahisisha utendaji lakini pia wakala zote zinapaswa kuwa kidigital ambao bado hamjaingia mnapswa kuingia na ambao mmeingia mnapaswa kuboresha hiyo miundombinu ili iwe shirikishi”amesema Simbachawene
Aidha Simbachawene amewataka watendaji wakuu kuhakikisha wanawapeleka vijana kwenye mafunzo ili kuwaandaa kuwa watendaji Bora wa baadae na sio kwenda wao kwenye mafunzo pindi yanapohitajika.
“Mimi niwaombe watendaji muwapeleke vijana kwenye mafunzo mara Kwa mara Kwani wao ndio wanaopaswa hasa kujifunza lakini sio nyinyi kule watapata “Exposure” hao ndio watu mtakao waachia ofisi”ameongeza Simbachawene
Amesema katika utawala Bora swala la maadili linapaswa kupewa kipaumbele hasa ukizingatia Teknolojia imekua hivyo kujitahidi kutojihusisha na maswala ya rushwa Kwani wao wanawakilisha serikali.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Utumishi Juma Nkome amesema wakala wameboresha huduma na kutanua wigo wa mapato hivyo kujitegemea wenyewe na kupata pesa za mfuko.
Amesema watendaji wakuu wanapaswa kutumia miongozo na mifumo mbalimbali iliyotolewa na wizara.
“Watendaji wakuu mnapaswa kutumia Tehama pia kutoa mchango stahiki kwenye pato la Taifa”amesema Nkome.