Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus (kushoto) akikabidhi Madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa Madawati.
Na Hellen Mtereko, Mwanza .
Kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Manispaa hiyo inakabiliwa na upungufu wa jumla ya madawati 3869 kwa shule za msingi hali inayosababisha changamoto ya kukaa chini kwa baadhi ya wanafunzi.
Akizungumza jana Julai 26,2023 kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 100 na Benki ya Nmb Mkuu wa wilaya ya Ilemela Hassan Masalla, amesema Manispaa hiyo inajumla ya wanafunzi elfu themanini na tisa mia mbili na saba wa shule ya msingi hali ambayo inasabisha upungufu wa madawati hayo ambapo halmashauri inaendelea kukabiliana na changamoto hiyo.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo Benki ya Nmb imekabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 9 kwa ajili ya shule za msingi Nyasubi na Kayenze ambapo Meneja wa benki hiyo Kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus, amesema hatua hiyo ni kuhakikisha taasisi hiyo ya fedha inashirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini na kuondoa changamoto kwa wanafunzi.
Baada ya zoezi hilo kukamilika baadhi ya wanafunzi wa shule zilizokabidhiwa madawati hayo Amon Charles na Neema wameishukuru benki hiyo kwa kuwasaidia kuondoa changamoto ya madawati huku wakimshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Elimu nchini.