Na Mwanshi wetu Jeshi la Polisi- Dar es salaam.
Wajumbe wa Mkutano wa askari Polisi wa Kike wa Duniani Ukanda wa Afrika (IAWP – International Association of Women Police – African Chapter) wameendelea na mafunzo na mada mbalimbali kufundishwa ikiwemo namna ya kukabiliana na wahalifu wanaojihisha na utakatishaji wa fedha Duniani.
Akitoa taarifa hiyo leo Julai 26,2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema mafunzo hayo yameendelea kutolewa na wawezeshaji kutoka nadani na nje ya Nchi ambapo wawezeshaji wamefundisha mada za mikakati ya mawasiliano, uongozi, utakatishaji wa fedha na ugaidi.
Kwa upande wake kamishna wa Polisi,Elice Mapunda-Mstaafu ambaye ni mwanamke wa kwanaza kufikia cheo cha kamshna wa Polisi amesema wao kama waanzilishi wa mtandao wa Polisi wa kike Tanzania TPF-net waliweza kuunganishwa katika Jumuiya ya IAWP i na kuwa wajumbe wa kudumu kitendo kilichopekea kufanikiwa Katika utekelezaji wa Majukumu ya Polisi.
Naye Kamishna Masaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi SACC Dkt. Noelia Myonga kutoka ofisi ya kiunganishi TANAPA Dodoma amesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa katika kutekeleza Majukumu yao.