Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa wakuu wa nchi za bara la Afrika kwenye mkutano wa kunadili changamoto kuhusu rasirimali watu unaofanyika kwenye ukumbi wa kiataifa wa Julius Nyerere leo Julai 26, 2023.
Baadhi ya Marais wa nchi za Afrika wakishiriki katika mjadala kuhusu changamoto zinazokabili Rasirimali watu na nini kifanyike kujenga mfumo mziri wa kulinda na kuendeleza Rasirimali watu barani Afrika kwenye mkutano unaofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere JNICC jijini Dar es Salaam
……………………….
Na Sophia Kingimali
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa nchi za afrika kuendeleza vijana kufikia ndoto zao ili kukuza rasilimali watu kwa maendeleo ya uchumi Kwa nchi.
Rais Samia ameyasema hayo Leo Julia 26 kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika wenye lengo la kujadili kuhusu mtaji wa rasilimali watu amesema Afrika Ina idadi kubwa ya vijana hivyo hiyo ni fursa ya pekee katika mageuzi ya uchumi.
“Idadi kubwa ya vijana tuliyonayo ni fursa ya kipekee katika ukuaji wa uchumi katika bara letu kuliko kuwaacha vijana Hawa kwenda kutafuta fursa ulaya na kupata tabu njiani tuwawezeshe Kwani Maisha Bora yapo Afrika”amesema Dkt Samia
Amesema swala la maendeleo ya rasilimali watu Afrika haliwezi kuja Kwa kubahatisha na Halima mbadala hivyo ni lazima kuweka mipango madhubuti kuhakikisha rasilimali watu Afrika inaendelezwa Kwa maslahi ya bara na maendeleo ya nchi.
Amesema katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linalinda na Kutunza rasilimali watu nchi imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kutenga Fedha kwenye Afua za lishe na kulinda Afya ya mama na mtoto lakini pia kuanzisha vituo vya watoto.
Ameongeza kuwa uanzishwaji wa mfuko wa kupunguza umaskini TASAF lakini pia mfuko wa kusaidia vijana kiuchumi pamoja na kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua.
Aidha Rais Samia amesema uwekezaji wa rasilimali watu ni wajibu wa kimaadili ili kujenga Afrika yenye uchumi wezeshi Kwa kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
Kwa upande wake Makamu wa rais wa Benki ya Dunia Dkt. Victoria Kwakwa amesema nchi za Afrika zinachangamoto kubwa ya elimu Kwani watoto wa Afrika kusini mwa jangwa la sahara asilimia 80 hawajui kusoma Wala kuandika.
Amesema maboresho katika sekta ya elimu yatasaidia kukuza mtaji wa rasilimali watu katika nchi za Afrika.
“Uganda imekua ya kwanza Kwa kuondoa udumavu kwenye maendeleo endelevu na Kenya imeboresha kwa asilimia 50 katika sekta ya elimu”amesema Kwakwa
Aidha Dr. Kwakwa ameipongeza Tanzania Kwa kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu Kwa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba shuleni baada ya kujifungua.
Sambamba na hayo amesema zàidi ya asilimia 50 ya walimu hawafundishi vizuri hivyo Kuna haja ya kutenga Fedha Kwa ajili ajili ya kuboresha miundombinu ya walimu ili kufikia maendeleo na kuboresha sekta ya rasilimali watu..