Na Sophia Kingimali
Pamoja na serikali kuweka sera ya elimu Bure bado Kuna maeneo nchini yamekuwa na changamoto Kwa wananchi kutopekeka watoto shule jambo ambalo ni kinyume na utaratibu na hii inapelekea upungufu wa rasilimali watu ambao Taifa linawategemea.
Hayo yamebainishwa leo Julai 25 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda baada ya kikao cha kiufundi cha mawaziri kutoka nchi za Afrika.
Profesa Mkenda amesema ili Tanzania iendelee yanahitajika mambo manne ambayo ni elimu, ardhi, afya na siasa safi.
Amesema dhana ya rasilimali watu ni watu wenye ujuzi, elimu na hurka ya kufanya kazi vizuri ni watu walio elimika, wanauelewa mpana na ujuzi wa kutosha.
“Kuwekeza kwenye elimu ni muhimu hivyo kila mzazi ni lazima awajibike kwa kusimamia mtoto ili apate elimu Kwani tunahitaji kuwekeza zàidi kwenye elimu ili twende sehemu nyingine Kwa kupata vijana wenye elimu ambao ndio rasilimali kubwa kwenye nchi yetu “amesema Profesa Mkenda.
Amesema rasilimali watu ni muhimu kwa maana hiyo wanaangalia kwa kutumia watu wenye Elimu na ujuzi wa kuendeleza uchumi katika taifa
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nala, Benjamin Fernandes amesema serikali iwekeze zaidi kwenye teknolojia kwa sababu duniani ya sasa kila kitu ni teknolojia.
“Nimeshiriki kwenye mkutano huu wa rasilimali watu kama kijana Kwani bado tunahitaji kuungwa mkono kwenye maswala mengi hasa kwenye teknolojia ambayo itasaidia nchi. Katika mambo mengi,”amesema Fernandes.