Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana akiwekewa mkono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mstaafu David Musuguri baada ya kumtembelea nyumbani kwake Butiama mkoani Mara.Kinana amefika nyumbani kwa Jenerali Musuguri ikiwa ni sehemu ya kumjulia hali na kutambua mchango wa Shujaa huyo.(Picha Zote na Fahadi Siraji wa CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mstaafu David Musuguri mwenye umri wa miaka 103 baada ya kumtembelea nyumbani kwake Butiama ikiwa sehemu ya kutambua mchango wa shujaa huyo wakati leo ikiwa Siku ya Maadhimisho ya Mashujaa. Katikati ni mtoto wa Jenerali Musuguri. (Picha Zote na Fahadi Siraji wa CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuzulu kaburi hilo leo ikiwa ni kutambua na kumkumbuka shujaa huyo namba moja kwa Taifa la Tanzania.Wengine katika picha hiyo ni viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama hicho. (Picha Zote na Fahadi Siraji wa CCM)
……………………………….
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amezulu kaburi la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kumtaka ni mwanamapinduzi wa kweli na shujaa wa Afrika.
Amesema wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya mashujaa, Mwalimu Nyerere anabaki kuwa shujaa namba moja wa Tanzania huku pia akimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali David Musuguli (103) na kumwelelezea ni alama ya uzalendo wa Taifa, ni alama ya ukombozi na anastahili kuombewa afya njema.
Kanali Mstaafu Kinana ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 baada ya kuzulu kqburi la Mwalimu Nyerere na kumtembelea Mzee Musuguli nyumbani kwake Butiama mkoani Mara akiwa katika ziara kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuzungumza na wanachama.
Akiwa katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na baada ya kuweka shada la maua, Kinana amemwelezea kuwa ni shujaa wa Tanzania na Afrika na kutoa mwito kwa nchi zinqzotamani kuzikalia nchi nyingine kiuchumi kuiga mema ya baba wa Taifa ambaye aliongongoza mapambano ya kumaliza udhalimu wa nduli Idd Amin nchini Uganda.
Aidha, akiwa nyumbani kwa Jenerali Musuguri, Kinana alimwelezea kuwa mzalendo wa kweli aliyeongoza mapambano dhidi ya Idd Amin.
“Jenerali Musuguli ameliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchibwa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, ameliongoza Jeshi katika nafasi mbalimbali, wakati leo tunaadhimisha miaka 44 ya vita ya Uganda Jenerali Musuguli ndiye aliyeyaongoza majeshi ya Tanzania kumng’oa Nduli Idd Amin.
“Ameliongoza Jeshi kwa zaidi ya miaka minane, Jenerali Msuguli ana nishani zote za juu za Jeshi, nishani zote kubwa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni alama ya shujaa, ni alama ya ukombozi, ni alama ya uzalendo wa taifa letu,” amesema.
Kanali Mstaafu Kinana aliyekuwa ameambatana na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Mara pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema kumjulia hali mzee Musuguli amesema amefurahi sana kuwa naye leo, ametimiza miaka 103 na kwamba anamtakia afya njema.