Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh. Tabia Maulid Mwita, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, wakati alipoondoka nchini kwenda Urusi ambapo atamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa Pili wa Kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi.