Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis akizungumza na Wakulima wa mradi wa Viungo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya usambazaji maji yalioyofanyika Ofisi za Mradi huo Mwanakwerekwe Zanzibar,julai 24,2023.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji Maliasili na MifugoZanzibar Shamata Shaame Khamis akikabidhi mipira wa maji kwa wakulima wa Viungo,mbogamboga na matunda wakati wakati wa makabidhiano ya vifaa vya usambazaji maji yalioyofanyika Ofisi za Mradi huo Mwanakwerekwe Zanzibar,julai 24,2023.
Mrajis Asasi za kiraia Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kilimo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kusambazia maji kwa wakulima wa mradi wa viungo yalioyofanyika Ofisi za Mradi huo Mwanakwerekwe Zanzibar,julai 24,2023.
Mkurugenzi mtendaji Community Forest Pemba Mbarouk Mussa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kilimo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kusambazia maji kwa wakulima wa mradi wa viungo yalioyofanyika Ofisi za Mradi wa Viungo Mwanakwerekwe Zanzibar,julai 24,2023.
……………………….
NA RAHMA KHAMIS MAELEZO
Jumla ya milioni 45 zimetumika kununua vifaa vya kumwagilia maji ili kuwanufaisha wakulima wa viungo,mbogamboga na matunda.
akikabidhi vifaa hivyo Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji Maliasili na Mifugo, Zanzibar Shamata Shaame Khamis huko Ofisi za Mradi wa Viungo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B’ amesema vifaa hivyo vitawasaidia vijana katika harakati za kilimo na kupelekea kujitoa kwenye kilimo cha kutegemea mvua.
Aidha amefahamiasha kuwa matangi ya maji pamoja na mipira iliyotolewa itasaidia katika harakati za umwagiliaji maji na kuhakikisha kua kilimo kinaimarika kwani wakulima wengi wataweza kufanya shuhuli zao bila ya kutegemea miongo ya mvua.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mashirika ya Maendeleo inapambana katika kuhakikiasha suala la Kilimo linaimarika kwani kwa mwaka huu bajeti ya Kilimo imefikia hadi bilioni 98.
Aidha Waziri huyo ameupongeza mradi wa viungo kwa kuwa wa kwanza kuanza harakati za kuwasaidia wakulima kwa mwaka wa fedha 2023-2024 jambo ambalo limesaidia kupunguza wimbi la vijana wasiojishuhulisha.
Aidha ameeleza kuwa uwepo wa Mradi wa Viungo na Wadau wengine umeongeza nguvu katika Serikali hivyo itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau hao ili kutatua changamoto zinzowakabili wakulima na wananchi kwa ujumla.
“Kwa wale vijana ambao wapo tu mtaani wanasubiri ajira nawaomba wajikite katika kilimo kwani kilimo cha sasa kimekua na tija kwa vijana wengi hivyo tushirikiane ili tulete maendeleo katika nchi nyetu” alifahamishaWaziri huyo.
hata hivyo waziri aliwataka Vijana kuacha kukaa vijiweni na badala yake kujishijishuhulisha na kilimo ili kujiletea maendeleo.
Nae Afisa katika mradi wa viungo Ali Said amesema kuwa vifaa hivyo vimewalenga wanufaika 50 wa mradi wa viungo ambao wanajishughuliha na kilimo cha umwagiliaji na hawana uwezo wa kununua matangi ya kuhifadhia maji.
“Tunaendeleza kuwapatia wakulima wa mradi wa Viungo vifaa mbalimbali ambavyo vitawasaidia kuhifadhia maji na kusambazia ili waweze kuendeleza kilimo na kujipatia kipato,” alifahamisha.
Mradi huo ni wa miaka minne na umewafikia wakulima 21 elfu ambapo hadi kukamilika kwake wanatarajia kuwafikia wakulima 57 Elfu Unguja na Pemba.