Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais, TAMISEMI Dk Charles Mahera akifungua ya mafunzo ya uongozi ,utawala na Menejimenti kwa viongozi wanaosimamia na kuendesha huduma za Afya,Ustawi wa jamii na lishe ngazi ya halmashauri na vituo vya kutolea huduma za Afya ,ustawi wa jamii na lishe mkoa wa Tanga ambayo yatawawezesha kujenga uwezo wa kusimamia na kuendesha huduma hizo.
Mkuu wa Taasisi ya CEDHA -Arusha ,Dk Johannes Lukumay akizungumzia mafunzo ya uongozi ,utawala na Menejimenti kwa viongozi wanaosimamia na kuendesha huduma za Afya,Ustawi wa jamii na lishe ngazi ya halmashauri na vituo vya kutolea huduma za Afya ,ustawi wa jamii na lishe mkoa wa Tanga ambayo yatawawezesha kujenga uwezo wa kusimamia na kuendesha huduma hizo.
……..
Julieth Laizer,Arusha.
Viongozi wanaosimamia na kuendesha huduma za Afya,Ustawi wa jamii na lishe ngazi ya halmashauri na vituo vya kutolea huduma za Afya ,ustawi wa jamii na lishe mkoa wa Tanga wamepatiwa mafunzo ya uongozi ,utawala na Menejimenti ambayo yatawawezesha kujenga uwezo wa kusimamia na kuendesha huduma hizo.
Akifungua mafunzo hayo leo yanayofanyika katika Taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya Watumishi wa Afya -Arusha ,Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais ,TAMISEMI, Dk Charles Mahera amesema kuwa,mafunzo hayo yana lengo la kujenga uwezo kwa timu za uendeshaji wa huduma za afya katika Halmshauri (CHMT) na vituo vya kutolea huduma (HMT) katika masuala ya uongozi, utawala na usimamizi wa rasilimali na ubora wa huduma ili kuleta tija na ufanisi katika uendeshaji wa vituo hivyo .
Dk.Mahera amesema kuwa,serikali imeendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini kwa kuzingatia sera ya Afya ya mwaka 2007 ambayo kwa sasa inafanyiwa mapitio,Mpango Mkakati wa tano wa sekta ya afya 2021-2026 .
Aidha amefafanua kuwa,pamoja na uwekezaji mkubwa uliopo, malalamiko kwa wateja juu ya ubora wa huduma yanaendelea kuwepo ,na Mh Rais wakati wa uingiaji wa mikataba ya lishe na Wakuu wa mikoa tarehe 30/9/2022 jijini Dodoma alitoa maelekezo tuweze kujikita kwa sasa katika kuboresha huduma na Ofisi ya Rais TAMISEMI wameandaa na wanaendelea kutekeleza mpango kazi wa uboreshaji wa huduma wenye maeneo mbalimbali ya kimkakati.
“Kupitia mafunzo haya mliyoyapata leo natoa rai mhakikishe mnatekeleza mambo tajwa na mhakikishe mnaenda kuyafanyia kazi kwani nimeambiwa mtatengeneza mpango kazi wa kuleta mabadiliko katika maeneo yenu ambayo naamini yatachangia katika utekelezaji wa maeneo yetu 11 ya kimkakati ya kuboresha huduma.”amesema Dk Mahera.
Aidha amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga Wakuu mikoa na Halmashauri Waganga Wafawidhi wa vituo na RHMT ,CHMT kuongeza uwajibikaji na kusimamia vituo hivyo ipasavyo na kuhakikisha fedha zote zilizopo vituoni zinatumika kwa wakati na kuzingatia mipango.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya CEDHA -Arusha,Dk Johannes Lukumay amesema kuwa, amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi hiyo ya CEDHA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wakifadhiliwa na GIZ .
Dk Lukumay amesema kuwa,mafunzo hayo ya wiki mbili watakuwa ni mwendelezo katika kanda zote za nchi hii na kuhakikisha wamefikiwa walengwa .
Amesema kuwa, Taaaisi hugo imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali kuhusu maswala ya Afya kwa lengo la kutatua changamoto za Afya na kutoa ushauri elekezi kuhusu maswala ya afya na kufundisha maswala ya utawala na uongozi.
“Leo tuna washiriki zaidi ya 43 katika mafunzo haya na tukimaliza hapa tunaenda kanda nyingine na mafunzo haya yanatolewa na Taasisi hii Tanzania nzima na mwisho wa siku washiriki hawa watakuwa wameelewa majukumu yao na hivyo kuweza kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.”amesema Dk Lukumay.