Na MWANDISHI WETU
Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia QS OMAR KIPANGA ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Bweni iliyopo kata ya Kanga wilayani Mafia mkoa wa Pwani iliyopaswa kukamilika mwezi July mwaka huu na hivyo kumtaka mkandarasi kukamilisha ujenzi wa shule hiyo kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa na serikali mpaka kufikia mwezi aug mwaka huu ili wanafunzi waendelee na masomo.
Naibu waziri OMAR KIPANGA ambae pia mbunge wa jimbo la Mafia amesema hayo wakati kukagua miradi mbalimbali inayojengwa katika jimbo la Mafia amesema bado hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa shule hiyo ambayo baadhi ya majengo yanajengwa kupitia fedha za mradi wa boost zinazotolewa na serikali kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo mpaka sasa zaidi ya milion 270 zimetolewa.
Nae mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Mafia KOMREAD MOHAMEDI FAKI pamoja na katibu wa chama wilayani OMARI MILONGE wakamtaka mkaguzi wa miradi kuhakikisha anatimiza wajibu wake ikiwemo kukagua kila hatua anayofikia mkandarasi ili ujenzi huo utakapokamilika uendane na thamani ya fedha zilizotengwa na serikali.
Hata Hivyo afisa elimu kata kanga YASSIN JUMBE amesema ujenzi huo ambao unataraji kukamilika mwezi aug mwaka huu utasaidia kuondokana na hatari ya kuangukiwa na kuta wakati wa masomo kutokana na vyumba vya madarasa kuta zake kuharibika vibaya.
Mwlm. YASIN JUMBE Afisa elimu kata.
QS KIPANGA alipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mingine ikiwemo barabara ya kilometa tano inayojengwa kwa kiwango cha changarawe ikiwemo kusikiliza kero za wananchi.