Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, Bw. Ashraf Roushdi, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu nia yao ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Mkutano huo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko, pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha. Mkutano umefanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, Bw. Davy Tharwat (Kulia), akitoa wasilisho la kampuni yake mbele ya ujumbe wa Tanzania, uliongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo Kampuni hiyo imeonesha nia yake ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Katikati ni Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo Bw. Ashraf Roushdi na kushoto ni Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Limu Holding ambaye ni mwekezaji mwenza wa Kampuni ya ORASCOM , Bw. Aloys Ntakirutimana. Mkutano huo uliofanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko, pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia), akizungumza jambo wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, kuhusu nia yao ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Mkutano huo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa tatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko (wa pili kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine (wa kwanza kushoto), na Kaimu Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (wa kwanza kulia). Mkutano umefanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, Bw. Ashraf Roushdi (katikati), akitoa wasilisho la kampuni yake mbele ya ujumbe wa Tanzania, uliongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambapo Kampuni hiyo imeonesha nia yake ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, Bw. Davy Tharwat na Kushoto ni Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Limu Holding ambaye pia ni mwekezaji mwenza wa Kampuni ya ORASCOM, Mhe. Aloys Ntakirutimana. Mkutano umefanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akiwa na Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Limu Holding ambaye pia ni mwekezaji mwenza wa Kampuni ya ORASCOM, Mhe. Aloys Ntakirutimana, baada ya kufanya mazungumzo kuhusu nia ya kampuni hiyo kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Mkutano umefanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya ORASCOM ya nchini Misri, uliongozwa na Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Bw. Ashraf Roushdi (wa tatu kulia), aliyeambatana na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Bw. Davy Tharwat (wa pili kushoto) na Rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Limu Holding ambaye ni mwekezaji mwenza wa Kampuni ya ORASCOM, Mhe. Aloys Ntakirutimana, baada ya kufanya mazungumzo yao kuhusu nia ya kampuni hiyo kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa nchini na mingine mipya. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa tatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko (wa kwanza kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine (wa pili kulia), na Kaimu Kamishna Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (wa kwanza kulia). Mkutano umefanyika Ofisi za Hazina Ndogo, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)