Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Bugarama wilayani Ngara mkoa wa Kagera wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo tarehe 23 Julai 2023. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi.
Wananchi wa Bugarama wilayani Ngara mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipofanya ziara wilayani humo tarehe 23 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo mara baada ya kuwasili katika mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoa wa Kagera tarehe 23 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto) akizngumza na Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha (katikati) alipowasili katika mgodi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoa wa Kagera tarehe 23 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza mara baada ya kupata taarifa ya maendeleo ya ulipaji fidia wananchi wanaopisha mradi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoa wa Kagera tarehe 23 Julai 2023. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathis Khabi.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha (kulia) akifuatilia uwasilishwaji taarifa ya ulipaji fidia wananchi wanaopisha mradi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoa wa Kagera wakati wa ziara ya Waziri wa Ardh Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula tarehe 23 Julai 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali Mathias Kahabi wakipata maelezo ya mradi wa uchimbaji madini ya Nickel wilayani Ngara mkoa wa Kagera tarehe 23 Julai 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………………………
mbalimbali za jamii. Hata hivyo, aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha wale wananchi wanaoenda kujengewa nyumba na kampuni hiyo wanawekewa mpango wa makazi utakaokuwa katika mpangilio wa kimji.
‘’Wale wananchi mtakaowajengea nyumba muangalie namna ya kuwapanga, tunahitaji upangaji wa kimji walau ufanane na mahali pale, mkiweza kuwasaidia mtawafanya wafanane kimji’’ alisema Dkt Mabula.
Kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited inatarajia kuchimba Madini ya Nickel katika eneo la Kabanga, Wilayani Ngara Mkoa wa Kagera ambapo zaidi ya hekta 4,000 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Januari 19 mwaka 2021 Serikali ya Tanzania na kampuni ya LIfezone Metals Nickel Limited zilisaini Mikataba uliowezesha kuanzishwa Kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited ambayo ni ya ubia kati yake na Serikali.