Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga akimkabidhi chetu cha ushiriki wa maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya kujiendeleza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), Dkt. Emmanuel Malisa, katika hafla ya ufungaji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julia 22,2023.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya kujiendeleza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), Dkt. Emmanuel Malisa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Ku malizika kwa hafla ya ufungaji wa maonesho ya Vyuo Vikuu iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julia 22,2023.
Bbadhi ya wanafunzi wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wahadhiri na watumishi katika banda la Cruz Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) katika maonesho hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya kujiendeleza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), Dkt. Emmanuel Malisa, akikabidhi cheti cha ushiriki wa maonesho hayo kwa Afisa Mawasiliano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Sokoine SUA, Bi. Suzana Magobeko mara baada ya hafla ya ufungaji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Julia 22,2023.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimejipanga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kutoa mafunzo ambayo yatawamsaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kujiajiri.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, katika maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2023, yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya kujiendeleza Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), Dkt. Emmanuel Malisa, amesema kuwa wanatoa mafunzo ya shahada za awali, uzamili, kufanya tafiti pamoja na kutoa ushauri wa kitaalama kwa wahitaji.
Dkt. Malisa amesema kuwa Chuo kinaendelea kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi jambo ambalo linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kujiajiri baada ya kumaliza mafunzo chuoni hapo.
“Vijana wengi wamekuja katika banda letu na wameona namna mafunzo yanavyotolewa kwa njia ya vitendo ambayo ni rafiki kwao katika kuhakikisha wanafikia malengo” amesema Dkt. Malisa.
Amefafanua kuwa katika kipindi chote cha maonesho wanafunzi zaidi ya 600 wamefanya udahili wa kujiunga na chuo kitu ambacho ni mafanikio kwao.
Naye Afisa Mawasiliano na Masoko wa Chuo hicho, Bi. Suzana Magobeko amesema Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ni Chuo bora kabisa na Kikongwe nchini Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki.
Amewataka wadau na wananchi wote kufika Chuoni kujipatia Elimu kuhusu masuala ya Kilimo na Mifugo ili kuongeza ujuzi zaidi katika shughuli zao
Ameongeza kuwa kwa wale wahitimu ambao hawakuweza kufika katika Maonesho ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia Mnazi Mmoja wanaweza kupata taarifa zaidi kwa kutembelea tovuti yetu www sua.ac.tz na ili kujisajili ingia http://197.250.34.38:8389/index.php/registration