Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati wa Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (Kushoto) na Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia), wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Katibu wa Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Twaha Mwakioja (kushoto), Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Bw. Muksini Mkumba (Katikati) na Afisa Mambo ya Nje (Foreign Service Officer) kutoka Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika, Bw. Nicholaus Joseph, wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kulia), akizungumza na Balozi wa Ghana nchini Kenya, Mhe. Damptey Bediako Asare (kushoto), ambaye amemwakilisha Waziri wa Fedha wa Ghana, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Mawaziri Mbalimbali wa Nchi 55 za Afrika, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Nairobi, Kenya)
……………………………
Na. Joseph Mahumi, WF, Nairobi
Tanzania imeshiriki Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, uliobeba kaulimbiu ya “Afrika baada ya Majanga”: Majadiliano juu ya Uwekezaji, Ukuaji Endelevu wa Uchumi na Ustawi kwa wote”. Mkutano huo uliojumuisha nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, umefanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
Akizungumza baada ya mkutano huo, Mhe. Chande alisema kuwa, Mkutano huo umekua na manufaa makubwa kwa Tanzania na Bara la Afrika kwa kuwa unatoa fursa ya kujadili masuala ya msingi katika mtangamano wa Afrika ikiwemo masuala ya Kodi, Mapambano dhidi ya Fedha Haramu; uanzishwaji wa Taasisi za Fedha za Afrika, uanzishwaji wa mfumo wa kidijitali wa uangalizi wa Uwekezaji, hatua muhimu na vichocheo vya kuiwezesha Afrika kufikia malengo ya maendeleo jumuishi na endelevu.
“Tanzania inaungana na nchi nyingine za Umoja wa Afrika kutoa mchango wake kwenye mijadala ya agenda kwa lengo la kufikia hatua muhimu za pamoja zitazowezesha kufanyika Mageuzi ya Kimuundo, Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika kupitia mikakati bunifu ya uwekezaji” Alisema Mhe. Chande.
Mhe. Chande aliongeza kuwa, katika Mkutano huo wamekubaliana kuweka kipaumbele zaidi katika Kukuza uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya kitaasisi na kisera inayohitajika katika kupata ufanisi kwenye jitihada za kufikia Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika pamoja na Kuja na Azimio la Mawaziri litakaloainisha mipango ya kisera na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika ngazi ya nchi, Banda na Bara ili kufikia Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika.
Aidha, Mhe. Chande ametumia jukwaa hilo kuwaalika Mawaziri hao pamoja na kuwashawishi Wakuu wao wa nchi, kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu masuala ya maendeleo ya Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Development Summit) utakaofanyika Dar es Salaam, tarehe 25 na 26 Julai 2023 chini ya uenyeji wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.